SIMULIZI :: Jini Mahabati Sehemu ya Ishirini na Mbili (Kwa wenye miaka 18+)
SIMULIZI : JINI MAHABATI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
MTUNZI: ManyamaJunior
AGE: 18+
ILIPOISHIA
Walifika hospitalini na moja kwa moja Radhia alishuka na kuingia kwa huyo dakatrai bingwa wa magonjwa ya wanawake. Alikuwa na hamu ya kujua kwa nini haoni mzunguko wake wa hedhi kwa mda mrefu sana au ndo tayari anaujauzito wa kijini. Akasema atajaribu kumueleza vitu vinavyomsumbua daktari huyo ili aone kama anaweza kumsaidia. Wakati anaingia tu simu yake ya mkononi ikaita.Kuangailia ilikuwa ni Tariq akipiga. Radhia akasita kuipokea. Mara ukaingia ujumbe mfupi wa maneno ukimueleza kuwa apokee simu kwani Tariq ana matatizo mazito..*****
SONGA NAYO.
Meseji hiyo ilimshtua sana Radhia na kujiuliza atakuwa amepatwa na nini tena. Akawaza haraka haraka akaona ngoja kwanza aonane na daktari alafu akitoka ndo atampigia. Akaingia kwenye chumba cha daktari. Akapewa ishara akae tayari kwa kupewa huduma. “Karibu sana binti unaweza tu kueleza tatizo lako” ilikuwa ni sauti ya pili ya daktari mara baada ya ile ya kwanza iliyohusu salamu. “Radhia akamwangalia kwa macho yake ya huba kabla ya kusema kuwa ana matatizo makubwa sana na hajui aanzie wapi kueleza. Dakatari huyo akatabasamu na kumwambia anzie mwanazo tu.
“Dokta mimi nimekua nikisumbuliwa na tatizo la kutoona siku zangu kwa mda mrefu sana na nimekua na wasiwasi sana. Ndo nimekuja kupata ufafanuzi kutoka kwako. “Vizuri sana vipi unashiriki tendo la ndoa kwa mda wote huo wa tatizo” aliuliza dakatri. “yeah nashiriki lakini sizani kama ni tatizo Radhia alijibu. “Yeah sio tatizo nimesema hivyo kwa maana labda unaweza kuwa na mimba daktari huyo alijaribu kufafanua. “Kwa hiyo daktari ukiachilia mbali kuwa ni dalili ya mimba kitaalamu tatizo la kutopata hedhi kwa mda mrefu linakuwaje Radhia aaliuliza. Swali zuri sana dokta alijibu huku akikaa vizuri kwenye kiti chake cha kuzunguka zunguka na kuanza kutoa darasa kidogo juu ya tatizo hilo.
“Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo. Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary). Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za sirini; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi. Hiyo ni ya kwanza lakini ya pili ni hivi akakoa kidogo na kupiga pafu moja la maji ya kunywa huku akimwangalia binti hyo kwa macho ya matamanio. Ujue tatizo jinni Barike aliambiwa aongeze spidi hivyo alikuwa akiwafanya wanaume wachanganyikiwe pindi wakutanapo na Radhia.
Sasa hapa dokta alishaanza kuyumba badala ya kueleza kwa kina tatizo la Radhia. Basi akaendelea kwa kusema hiyo hali ya pili inayoitwa sekondari amenorrhea.
“Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.
“Eeeeeh hiyo ndo linalonikumba mimi” alidakia Radhia.
“Ni kweli unaweza kuwa kwenye kundi hili lakini ngoja nikueleze jinsi hedhi inavyotokea…
“Sawa dakatari nileleze jinsi mwanamke anavyopata hedhi .
“Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus napituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa” Dakatari huyo alifafanua kwa mbwembwe za kitaalamu.
“Sawa daktari nimekulewa lakini hujanambia Amenorrhea husababishwa na nini? Radhia aliendelea kuuliza maswali yake ya udadisi.
“Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke”. Alifafanua daktari huyo.
“Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary. Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na (Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary, Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi, Lishe duni na utapia mlo pia bila kusahau Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza) vyote hizi vya weza kuwa ni tatizo
“Matatizo Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamu Prolactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary. Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary, Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua, Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili vyote kwa pamoja vinachangia tatizo la kutopata damu ya hedhi. Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary. Nayo pia huachangia. Hapo Radhia akawa anasikiliza haelewei na tayari ule muwasho wake ulishanza kumsumbua.
“Kitu cha mwisho ambacho ningependa kukifafanua ni Matatizo katika ovary” Daktari alisema huku akiamkazia macho Radhia mana alikuwa kama amebadilika ghafla. Alikuwa amelegea sana kama mtu ambaye alipandishwa hisia za mapenzi na kuachwa bila kupewa dozi.
“Vipi tupo pamoja? aliuliza daktari huyo.
Radhia akawa kama ameshtuka kutoka usingizini na kumwambia “endelea”.
“Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation),Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu(Hyperandrogenemia), Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa”alisema dokta huyo.
Radhia aliendelea kukaa kimya hivyo daktari akaendelea kuonesha utaalamu wake. “Pia kuna sababu zingine kama Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake bila kusahau, Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao huambatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida. Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (geneticdisease).
Sijui hata huyu dakatari kwa nini aliamua kueleza vitu vyote hivyo ili hali mwenzake alikuwa katika hali mbaya na alitamani dokta amwambie amchunguze hasa hizo sehemu za muwasho. “Alafu daktari mbona matatizo ya ovary yamekua na maelezo mengi alijaribu kusema Radhia ili dokta huyo akatishe maelezo na ikibidi ampe dawa ya mshawasha uliokuwa ukimsumbua.
***ITAENDELEA***
No comments:
Post a Comment