Trending News>>

Msaada: Amenikataa Na Kaniachia Ujauzito


Mimi ni binti niliyehitimu elimu ya chuo kikuu miaka ya nyuma kidogo wakati nikiwa chuoni kuna kijana alinipenda sana akanifuatilia kwa mda baada ya semister ya kwanza kuisha nilimkubalia tukaanzisha mahusiano na tulipendana sana chake kilikuwa changu na changu chake tulikuwa na ndoto nyingi sana za kutimiza ikiwemo kuoana.
Mwezangu alikuwa na wivu sana kwakweli alikuwa ananichunga mno kila sehemu mpaka simu hali iliyopeleka kila mwanaume aliyenitongoza kumtukana hivyo kunifanya nisiwe kabisa na urafiki ‘na wanaume nilifanya hivyo sababu nilichoka ugomvi wa kila Mara hivyo tuliishi maisha ya kama mume ‘na mke kipindi tupo chuoni mpaka tunamaliza na nilijitoa kwa mengi sana maana nilikuwa shajua huyu ndio mume wangu hivyo suala la mahusiano kwangu sikuwa naliwaza tena zaidi ya kuwaza mambo mengine kwavile ‘na yeye alinijengea mazingira ya hivyo.
Tulipomaliza chuo mwezangu alikuwa ashaanza process za kuomba kazi ikatokea akapoteza simu yake akaniomba nimwachie smartphone yangu pamoja na laptop kwavile anahitaji kuwa katika ulimwengu wa mtandao kuapply kazi Ikiwa na kuniandalia mimi CV pia atakuwa ananiombea ajira nikamwachia mimi nikawa ‘na kisimu cha tochi nikasafiri kurudi kwetu nikimwacha yeye jijini.
Nikiwa kwetu sikuwa kwenye mtandao kabisa sababu ya kisimu cha tochi ‘na mwezangu alibadilika akawa hanitafuti tena kama zamani kitu ambacho kiliniumiza sana na nikimwambia anafoka yuko busy nk, nikawa navumilia tu kumbe alikuwa keshapata ajira nzuri tu kwenye kampuni nzuri tu wala hakuniambia.
Siku moja mida ya usiku nilishika simu ya dada yangu nikaamua kuchungulia insta nikaamua kumtafta uzuri a/c yake haikuwa private nikampata lakini sikuamini nilichokutana nacho baada ya kukuta ana mwanamke tena wanakula bata si za nchi hii kila sehemu anampost my wife, my everything nk kwakweli sitaisahau hiyo siku nililia kwa maumivu yote nikiwaza.
Mara nyingi tu mimi nilimtaka tuachane kutokana na tabia ya wivu uliopitiliza mpaka kunipiga lakini alikuwa hataki, pili amepata kazi akaniona mie sifai kuspend nae hizo pesa akatafuta binti wa chuo mie niko huku nasubiri hata apate hela anunue simu anitumie smart phone yangu japo niwe mtandaoni kusaka ajira.
Kumbe mwezangu hana habari lakini kilichoniuma zaidi bora hata angeniambia basi kuliko nimejitunza najua nina mpenzi kumbe yeye anamwingine kiufupi iliniathiri sana home maisha magumu ndio kipindi hicho magu kashika nchi.
Ajira ngumu basi nilikuwa mtu wa kulia tu nikadhoofu sana kwa mawazo kitu kilichonifanya kujiingiza kwenye mahusiano mengine bila kuchukua muda kumjua mtu alivyonitongoza tu nikakubali kupunguza stress.
Nikiri niliweza kumsahau kwa haraka sana huyo mpenzi wangu nilijiaminisha nina furaha huku niliko ilikuwa furaha ya mwanzo tu bora hata nisingeingia kwakweli nilikoingia ndio ilikuwa balaa kuliko huko mwanzo alikuwa mkaka mtanashati mwenye kazi yake nzuri tu ukimuona utasema ni gentleman kumbe ni playboy vibaya mno jamani sidhani kama kuna sketi inampita huyu jamaa nilikuwa nimeingia kwenye stress nyingine mpya kabisa.
Pamoja na yeye kuwa na kazi yake sikuwa naijua sent kumi yake hata nauli tu za kumeet zote nilikuwa natumia vijisenti vyangu na hapo sina ajira, niseme tu ukweli kutokana na mazingira niliyokulia sijui kuomba yaani mtu asipojiongeza ndio basi siwezi omba naona jamaa akawa ameona hapa ndio pazuri haombwi hela basi hajiongezi hata siku moja hajawahi nipa senti yake ni mtu selfish sana anayejijali mwenyewe tu mtapanda daladala atakusubiria ulipe jamani.
Nikiri kabisa hapa nilijua sipendwi lakini nilishindwa kuondoka nilikuwa naogopa sana kuwa mpweke tena nilijifariji kwa kujiambia nitaondoka nikipata mtu anayenipenda hivyo nikaendelea kubaki kila siku ni zaidi ya Jana, jamaa nikawa namfuma mara nyingi tu ‘na wanawake kwake alipopanga na haombi msamaha ila mimi ndio narudi tena kuomba turudiane ‘na akawa amejua siwezi ondoka ndio kabisa vituko vikazidi na wala hajali duuh sijawahi kudate mwanaume kama huyu, jeuri, mbinafsi katili yaani huwa najuta siku niliyokutana na huyu mkaka nailaani kabisa.
Haya yaliyonipata leo ni matokeo ya kutofanya maamuzi magumu ya kuondoka najua mimi ni mjinga tena wa mwisho kabisa duniani hatimae pasipokujua nilikuwa na mimba hapa naomba niseme katika maisha yangu sijawahi shika mimba ‘na hospitali nilishaambiwa siwezi zaa kwa hiyo suala la mtoto halikuwahi kuwa akilini mwangu na sikuwahi kushika ujauzito hili lilinichanganya kidogo kwakweli .
Ukizingatia mtu niliyenae nilijua kabisa nikimwambia moja moja ataniambia nitoe hilo nililijua wazi hivyo nikafanya kama kumpa taarifa tu ‘na kweli kama nilivyotarajia akaniambia nitoe moyo wangu haukutaka kabisa hicho kitu nikamjibu siwezi fanya kitendo hicho akasema kama sitoi yeye hahusiki kwa lolote nisimjue ever nami nikakubali kwa kusema poa na huo ndio ukawa mwisho wa mawasiliano yetu.
Nilikuja kujua jamaa ni mume wa mtu na ana watoto watatu kitu kilinishtua sana mana anaishi kama bachelor tena alinambia yeye kamaliza chuo ndio kapangiwa kazi huku mkoa niliopo kwamba ni single akanipa ‘na story nying tu za uongo, huku ni kweli hana ndugu mana kaletwa kikazi kumbe alikotoka kaacha mke ‘na watoto nikimwangalia mkewe kwa mtandao huwa namuonea huruma tu kuwa na mume malaya kiasi hiki anaishi kibachalor hajawahi hata post picha ya mwanae.
Hiyo ilifanya nielewe mambo mengi sana lakini kikubwa kuliko yote ilibidi nikubaliane na hali yangu kuwa naenda Kuwa single mom nimefight sana kupata ajira bila mafanikio kila nikipita maofisini maboss wanataka wakutumie ndio upate ajira mana mimba changa hata huwa haionekani na sikuwa tayari kwa hilo ninampenda sana mwanangu kiasi cha kutokubali kufanya mapenzi na mwanaume mwingine yeye akiwa tumboni sijui naonaje lakini ndio hivyo hiyo imefanya nisipate kazi hasa mpaka nimekata tamaa ya ajira.
Nimekuwa mtu wa kulia tu yaani machozi kwangu ni kama maji ya kunywa kila siku najiuliza sijui nina mkosi ama laana gani jamani nimelia mpaka nahisi moyo wangu sasa umeota sugu nikitaka kulia tu najiambia hata nikilia machozi hayaleti pesa basi nanyamaza.
Na kwa bahati mbaya mzee wetu alitukuza malezi yale huruhusiwi hata kwenda kwa jirani hivyo ni mtu ambae nimekuwa maisha ya kivyangu kukaa ndani tu hata nikiwa chuoni sikuweza kutengeneza marafiki nilikuwa mtu wa movie tu hostel ukiondoa hilo ukoo wetu ni ule kila mtu na familia yake huwezi pata shida ukasema uende kwa ba mdogo ama shangazi ama ba mkubwa sijui wanamatatizo gani.
Lakini kila mtu yuko kivyake na familia yake kila mmoja akijaribu kuonyesha yeye ni bora ya mwenzie maisha yalivyo magumu nilikuwa natafuta vibarua mpaka vya kubeba mchanga japo upate elfu mbili lakini kadri siku zilivyoenda ikashindikana mana nakosa pumzi kutokana na ujauzito hivyo naishia kupumzika na kulala.
Mwanangu ananifanya niwaze kufanya chochote japo apate hata uji ama mavazi akija ndio kisa kimenifanya niombe msaada hapa JF naamini kuna watu wengi kwayeyote anayeweza kunisaidia mtaji nijishughulishe na chochote namuomba tafadhali tuwasiliane imenibidi tu nivae ujasiri nije kuomba hata nisipopata wa kunichangia angalau nimejaribu kuliko kukaa kimya.
Sina msaada wowote kwa sasa hata kula tu ni shida aisee lakini namshukru Mungu tunaamka salama na afya njema ninayo japo hata click sijaanza miezi mitano sasa ila naamini niko salama mimi ‘na mwanangu pia nikiamini hili nalo lita pita.
Mungu awabariki samahani kwa story ndefu ila nimefupisha mengi mno.

No comments:

Powered by Blogger.