Trending News>>

Ubigiji yatokea mlango wa nyuma

Timu ya taifa ya Ubeligji imefanikiwa kutokea nyuma kwa mabao 2 na kushinda kwa 3-2, mchezo wake wa raundi ya 16 bora dhidi ya Japan uliomalizika usiku huu huko mjini Rostov Urusi na kuifikia rekodi ya Ureno ya mwaka 1966.


Jumanne , 3rd Jul , 2018


Na Elbogast Myaluko



Wachezaji wa Ubeligji na Japan wakigombe mpira wa juu ambao ulizalisha bao la pili la Ubeligji.

Ureno iliweka rekodi ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 5-3 ndani ya dakika 90 kama walivyofanya Ubeligji leo. Ureno yenyewe ikiwafunga Jamhuri ya Korea kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966.


Mbali na rekodi hiyo ya Ureno, Ubeligji pia imevunja rekodi ya Ujerumani ya mwaka 1970 ambapo ilitoka nyuma kwa mabao 2 na kushinda dhidi ya England lakini wao wakishinda ndani ya dakika 120 lakini Ubeligji wameshinda ndani ya dakika 90.

Mabao ya Japan ambayo yaliwashangaza wengi leo yalifungwa kwa haraka haraka kipindi cha pili kupitia kwa Genki Haraguchi dakika ya 48 na Takashi Inui dakika ya 52. Ubeligji walisawazisha kupitia kwa Jan Vertonghen dakika ya 69 na Marouane Fellaini dakika ya 72 kabla ya Nacer Chadli kufunga bao la 3 dakika ya 90.

Ubeligji sasa watakutana na mabingwa mara 5 wa Kombe la Dunia Brazil katika hatua ya robo fainali. Brazil waliwafunga Mexico mabao 2-0 kwenye mechi ya mapema.
 

No comments:

Powered by Blogger.