Zinedine Zidane aipeleka Real Madrid fainali ya 3 mfululizo
Real Madrid wameweka rekodi mpya hii leo baada ya kufudhu kwenda fainali ya Champions League kwa mara ya 16, huku Zinedine Zidane akiwa kocha wa kwanza kufudhu kwenda fainali hizo mara 3 mfululizo baada ya Marcelo Lippi 1996-1998.
Dakika ya 3 tu Joshua Kimmich aliwanyanyua kwenye viti mashabiki wa Bayern Munich baada ya goli la utangulizi, goli ambalo limemfanya Kimmich kuhusika katika mabao 7 ya Bayern Munich katika CL msimu huu(kafunga 4 na assist 3).
Goli la kusawazisha la dakika ya 11 la Karim Benzema limekuwa goli la pili msimu huu wa Champions League kufungwa baada ya kupigwa pasi nyingi(28), ni bao la Lucas Digne pekee ndilo ambalo zilipigwa pasi nyingi kuliko hili(29).
Karim Benzema aliongeza bao la pili dakika ya 46 na hii kuwa mara yake ya kwanza kufunga mabao 2 katika mechi moja ya Champions League tangu afanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2014 vs Schalke 04.
James Rodriguez dakika ya 63 aliufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-2 na sasa anakuwa mchezaji wa saba katika historia ya Champions League kuwahi kuifungia pamoja na kuifunga Real Madrid, sasa Madrid wanafudhu kwa aggregate ya bao 4-3.
No comments:
Post a Comment