RAIS MAGUFULI AHIMIZA NIDHAMU NA UWAJIBIKAJI KWA WAFANYAKAZI.
Iringa. Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, amewahimiza wafanyakazi wote nchini kuzingatia nidhamu na uwajibikaji wawapo katika sehemu zao za kazi.
Rais Magufuli ameyasema hayo jana mjini Iringa wakati akihutubia kwenye sherehe za mei mosi ambazo kitaifa zilifanyika mkoani humo.
“Nidhamu na uwajibikaji kwa wafanyakazi ni jambo la msingi sana”, amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema wafanyakazi ambao ni wazembe na wavivu wamekuwa hawatoi mchango unaotakiwa katika maendeleo ya taifa, na hivyo kuwaita wafanyakazi wa aina hiyo ‘wanyonyaji’.
“Mtumishi au mfanyakazi akiwa mzenbe na mvivu atashindwa kutoa mchango kwa taifa, lakini anakuwa ni mnyonyaji”, ameongeza Rais Magufuli.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema serikali yake imefanikiwa kuajiri watumishi 18801 tangu iingie madarakani, ambapo katika idadi hiyo walimu ni zaidi ya 6500, na watumishi katika kada ya afya wakiwa 3652, huku idadi iliyobaki akisema ni kutoka kada nyingine.
“Tangu tuingie madarakani hadi hivi sasa tumeajiri watumishi 18801, kati yao walimu zaidi ya 6500, watumishi wa afya 3652, na waliobaki ni kada nyingine”, amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameahidi kuboresha maslahi ya wafanyakazi mara baada ya zoezi la uhakiki na kuajiri watumishi wapya litakapokamilika.
No comments:
Post a Comment