Trending News>>

CCM YAWAVAA WAZAZI WANAOSHAWISHI WATOTO KUTOENDELEA NA MASOMO


Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Simiyu imewaonya baadhi ya wazazi wanaowashawishi watoto wao kuandika majibu yasiyo sahihi kwenye mtihani wa Taifa wa darasa la saba ili wasiendelee na masomo ya sekondari.
Onyo hilo limetolewa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Simiyu, Jumanne Mganda katika kikao cha baraza la jumuiya hiyo kilichofanyika jana mjini Bariadi.
Mganda alisema vitendo hivyo vinawanyima fursa watoto kuendelea na masomo ya sekondari na ya elimu ya juu. 
Naye Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Donald Magessa amewataka wajumbe wa jumuiya hiyo kufuatilia mali za chama katika maeneo yao.

No comments:

Powered by Blogger.