Trending News>>

AZAM FC YAPANGA KUMDHALILISHA YANGA LEO


WACHEZAJI wa Azam FC wamepanga kwanza kumzuia Obrey Chirwa wa Yanga asilete madhara katika mchezo wao wa leo pia wamepanga kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.

Leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Azam itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Beki wa kati wa Azam, Aggrey Morris, amesema Chirwa ni straika wa kawaida kama walivyo wengine, hivyo amejipanga kumzuia watakapokutana leo.

“Nimejipanga vizuri kuhakikisha timu yangu inapata matokeo mazuri bila ya kuhofia mtu yeyote. Chirwa ni mshambuliaji wa kawaida kama walivyo wengine, hawezi kunisumbua, nimejipanga kumdhibiti,” alisema Morris. Naye nahodha wa Azam, Himid Mao alisema; “Ukiiangalia Yanga ilivyo kwa wakati huu, haiwezi kuwa kigezo kwetu kuwadharau zaidi ni kuangalia tunashinda vipi basi.”

No comments:

Powered by Blogger.