Trending News>>

AUNT LULU AMPA PAPII OFA YA PENZI

Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’.
MWANADADA aliyewahi kuwa mtangazaji ambaye haishiwi na matukio, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amesema kuwa yupo tayari kumpa ofa ya mapenzi mwanamuziki Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ mpaka asahau maisha aliyopitia.

Akiongea na Risasi Jumamosi, Aunt Lulu alisema amemuona Papii amekuwa mpya na anapendeza kila kukicha hivyo amejitolea kumpatia penzi iwapo atamkubalia ili asahau kabisa shida za dunia.
Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
“Unajua mimi najua kupenda, iwapo nitampatia penzi Papii mbona atasahau kabisa alipotoka, yeye akubali tu maana sijawahi kuona mahusiano yake, naamini kwa kipindi alichokaa jela kama angekuwepo mwanamke angejitokeza lakini haijawa hivyo, mimi nipo kwa ajili yake,” alisema Lulu.

Mwandishi wetu alijaribu kumpigia simu Papii ili kumfahamisha juu ya ofa hiyo ya mapenzi lakini hakuweza kupatikana mara moja.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

No comments:

Powered by Blogger.