Trending News>>

WAZIRI NDALICHAKO AWAONYA WANAOPOTOSHA SERA ELIMU BURE

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka watu kuacha kupotosha kuhusu sera ya elimu bure kwa kuwakataza wananchi kuchangia maendeleo ya elimu.
Prof. Ndalichako ametoa wito huo jana Mkoani Njombe ambako yuko kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu.
Alisema kuwa, waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016 na namba tano wa 2015 una ainisha kwamba wazazi na kamati za shule zinaweza kujiwekea utaratibu kwa wanaotaka kuchangia vitu vya shule ikiwemo chakula.
Prof. Ndalichako alisema, serikali imekataza walimu kujikita katika kukusanya michango ya hiari ya wazazi inayochangwa kwa sababu mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.