WADAU WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSI.
Imeelezwa
kuwa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kutapunguza uhalifu
unaohatarisha amani na kuongeza usalama wa mtu, jamii, nchi na dunia
kwa ujumla.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amesema hayo katika kikao cha wadau cha
kupitia mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi
na kusisitiza umuhimu wa kujielimisha kabla ya kusambaza taarifa.
“Ni
muhimu kwa jamii kuelewa haki ya faragha ya mtumiaji wa mawasiliano na
namna ya kushughulikia taarifa katika ukusanyaji, usambazaji, uchakataji
na uhifadhi ili kuepuka kutenda uhalifu” amesema Dkt. Sasabo.
Dkt.
Sasabo amezungumzia umuhimu wa jamii kuzingatia sheria ya makosa ya
mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka
2015 ili kuepuka makosa yasiyo yalazima na kuepuka usambazaji wa taarifa
binafsi za watumiaji wa mawasiliano usiouwiana na maadili na wenye nia
ovu.
“Ni
vema jamii ikajua mitandao haina mipaka, hivyo ni muhimu kuwa na
muongozo utakaosimamia haki za watumiaji na kulinda taarifa binafsi”,
amesisitiza Dkt. Sasabo.
Naye,
Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, amesema
mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamechangia ongezeko kubwa la makosa
katika mawasiliano ya simu na intaneti hivyo uwepo wa sheria
inayosimamia taarifa binafsi utapunguza changamoto za kimtandao na
kuongeza haki ya faragha.
Dkt.
Sasabo, alikuwa katika kikao kazi cha wadau kukusanya maoni ya
mapendekezo ya kutungwa sheria ya kulinda taarifa za watumiaji ili
kupunguza uhalifu na kuhakikisha usalama wa taarifa binafsi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Afisa
Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, akisisitiza jambo
wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa
binafsi, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Usalama Mtandao,
Eng. Stephen Wangwe.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa
siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani
Dodoma, leo.
Wadau
wa Sekta mbalimbali, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo
(hayupo pichani), wakati wa mkutano wa maoni kuhusu sheria ya kulinda
taarifa binafsi,Mkoani Dodoma, leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akiwa katika picha ya pamoja na sehemu
ya wadau walioshiriki katika mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria
ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,.
No comments:
Post a Comment