TMRC YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KIWALANI
Kampuni
ya Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC), imetoa zawadi ya
Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili (Shilingi
2,000,000) kwa Kituo cha Watoto yatima cha Kiwalani (Kiwalani Orphanage
Centre) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Zawadi
hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bw. Oscar P.
Mgaya kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji Elias Mwakalukwa -,
katika ghafla iliyofanyika kwenye Kituo hicho kilichopo jijini Dar es
Salaam.
Miongoni
mwa zawadi zilizotolewa kwa kituo hicho cha watoto yatima ni pamoja na
mchele, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage, sabuni za kufulia na
kuogea, sukari , chumvi, dawa za meno, majani, kalamu na madaftari
“Kwa
upendo wetu wa dhati kabisa tumeona umuhimu wa kushiriki pamoja na
watoto yatima, ambao wapo katika mazingira magumu, katika kusherehekea
Sikukuu ya Krimas mwaka 2017,” alisema Bw. Mgaya.
Bw.
Mgaya, alisema kuwa taasisi yake imeamua kujumuika na watoto hawa
yatima katika kuelekea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa kutoa zawadi
mbalimbali za vyakula kama njia ya kuwafanya wajisikie furaha.
Hata
hivyo, Mtendaji Mkuu huyo, amezitaka taasisi nyingine na watu binafsi
kujitoa kwa dhati kuwasaidia watoto walioko maeneo mbalimbali nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji Elias Mwakalukwa,
ameishukuru TMRC, kwa msaada huo na ameziomba taasisi nyingine kuiga
mfano wao.
“Tunaishukuru
sana TMRC, ninyi mmeonyesha mfano na hakika mmeonyesha upendo wa dhati
kwa watoto hawa. Niziombe taasisi nyingine kuchukua mfano huu uliofanywa
na taasisi yenu,” Mchungaji Elias Mwakalukwa alisema.
Aliongeza
kuwa uhitaji wa misaada kwa kituo chake ni mkubwa, lakini taasisi yao
inapata faraja kupata wadau wanao ona umuhimu wa kusaidia watoto hao
yatima.
No comments:
Post a Comment