Fifa Yazuia Usajili wa Kwasi
Baada ya mtandao huo kushindwa kufanya kazi mpaka jana mchana, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefunguka kwa kusema muda wowote mtandao huo utakapokuwa sawa, Fifa watatoa saa 24 kwa timu zilizofanya usajili kumalizia taratibu zao za usajili.
Kutokana na hali hiyo, jina la Kwasi raia wa Ghana na wachezaji wengine wote waliosajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo, kwa sasa hayatambuliki na Fifa mpaka pale mtandao huo utakapokuwa sawa.
Hata hivyo, usajili wa wachezaji wa kimataifa bado unaendelea mpaka keshokutwa Jumatano.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema: “Ni kweli mpaka tunavyoongea hivi sasa saa saba mchana (jana Jumapili), bado hatujapata taarifa za mtandao huo kuwa sawa, lakini muda wowote tukipata taarifa tutazijulisha klabu zote kuthibitisha usajili walioufanya ndani ya saa 24 kwani hakuna jina ambalo limeshaingia kwenye mfumo mpaka sasa.
“Ieleweke kwamba muda wa usajili hautaongezwa kama wengi wanavyodhani, sisi usajili tulifunga Desemba 15, kwa hiyo wale wote waliowasilisha majina yao ndani ya muda ndiyo watakaohusika na huo muda wa saa 24 ambao Fifa watakaoutoa, kinyume na hapo hakuna mchezaji mpya atakayeongezwa mpaka kipindi kijacho cha usajili.
“Fifa wanafanya juhudi kubwa za kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa kwani mafundi wao huko Uswizi wanahangaika wakati wote, hivyo tunaamini haitachukua muda mrefu mambo yatakaa sawa.”
Omary Mdose, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment