VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA
Said Mwishehe, Blogu ya jamii
MWENYEKITI
wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(TID) Profesa
Apollinaria Pereka amewataka vijana wasisite kuanzisha viwanda nchini
kupitia elimu ya ufundi waliyoipata kwenye taasisi hiyo kwa manufaa ya
taifa.
Pia amesema wasiogope changamoto watakazokumbana nazo na badala yake wawe wabunifu katika uanzishaji wa bidhaa zao.
Profesa
Pereka amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye Mahafali ya 11 ya DIT
ambapo amefafanua ,Serikali imejipanga kupiga vita umasikini, hivyo
vijana ni vema wakaanzisha viwanda ili wajiajiri wenyewe.
Amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kulijenga taifa na kuanzisha viwanda endelevu.
Ameongeza
nchi yenye maendeleo makubwa ni ile yenye ujuzi wa ufundi,na wanaotumia
teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uwanzishaji wa viwanda.
Pia amesema kwa sasa DIT imefikisha miaka 60 tangu ianzishwe na imefanya kazi kubwa kueneza elimu ya ufundi nchini.
“Utimizaji
wa miaka 60 ya DIT imeenda sambasamba na serikali ya awamu ya tano ya
kuanzisha viwanda nchini kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi ,hivyo
tutakwenda sambamba na serikali hiyo ili kutimiza azma ya Rais, Dk. John
Magufuli,"amesema
Awali
Mkuu wa chuo hicho Profesa Preksedius Ndomba,amesema Serikali ya awamu
ya tano inalenga kuleta maendeleo ya viwanda vidogo,vya kati na
vikubwa.
"Hivyo vijana wajiunge katika vyuo vya ufundi ili kuweza kupata ajira na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.
“Elimu
ya ufundi ina umuhimu mkubwa katika serikali hii ya awamu yatano kwa
sababu ya uwanzishaji wa viwanda nchini, vijana mjifundishe ufundi
sanifu kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe”amesisitiza Profesa Ndomba.
Ameongeza
DIT ipo sambasamba na Serikali katika kufanikisha uanzishwaji wa
viwanda, hivyo wapo makini katika utoaji wa elimu yao ili vijana wao
wakimaliza wawe wasanifu wazuri katika viwanda vinavyokuja na kwamba
wataendelea kupia watalaamu.
Mwenyekiti
wa Baraza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), Prof. Apollinaria
Pereka akizungumza kwenye Mahafali ya 11 ya taasisi hiyo jijini Dar es
Salaam ambapo jumla ya wahitimu 876 wamehitimu ngazi mbalimbali za
kitaaluma za Stashahda, Shahada na Shahada za Uhandisi na Teknolojia.
No comments:
Post a Comment