Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) ambao ulikua
ufanyike leo umesogezwa hadi kesho kupisha mashauriano yatakayofanywa
na baraza la mawaziri wanachama wanaohusika moja kwa moja na Jumuiya ya
Afrika Mashariki(EAC) baada ya mbunge kutoka Uganda, Freddy Mbidde
kupinga Tanzania kuwa na mgombea.
Chanzo cha mgogoro huo kinadaiwa ni Tanzania kuwa na mgombea wa nafasi
ya Uspika, Adam Kimbisa wakati nafasi hiyo huwa ni kupokezana na Spika
wa kwanza wa Eala, Abdulrahman Kinana alitoka Tanzania akifuatiwa na
Kenya kisha Uganda.
Mbidde ametoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge kutokana na akidi kutotimia
wakati wa kufanya uchaguzi licha ya wabunge kutoka nchi zote sita kula
kiapo cha utii mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Madete.
Baadaye ilibainika wabunge wengi wa Tanzania na Burundi hawakuwemo
kwenye ukumbi wa bunge na Mbidde kuomba kutoa muda wa mashauriano zaidi
ili kuruhusu nchi zinazostahili kuwa na wagombea kufanya hivyo ambazo ni
Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.
Hata hivyo hadi jana wagombea wa nafasi hiyo walikua watatu ambao ni
Adam Kimbisa, Leontine Nzeyimana ambaye ni Waziri wa zamani Afrika
Mashariki wa Burundi na Mwendesha mashtaka Mkuu mstaafu wa Rwanda, Dk
Martin Ngoga huku Sudani Kusini ambaye ni mwanachama mpya katika jumuiya
hiyo haikutoa mgombea.
Katibu wa Bunge, Kenneth Madete ameahirisha bunge hadi kesho saa 8:30
mchana kwaajili ya kumchagua Spika na baadaye makamishna na kuunda
kamati mbalimbali zitakazosaidia kutekeleza majukumu ya bunge hilo la
nne.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dk
Suzane Kolimba amekiri kuwa baraza la mawaziri watakutana kushauriana ni
njia ipi itumike kabla ya uchaguzi wa kumpata Spika wa nne.
"Kumetokea kutokuelewana na sisi baraza la mawaziri tutakutana
kushaurina namna ya kusonga mbele katika hali hii na uchaguzi utafanyika
kama mnavyojua suala la akidi ni muhimu katika vikao vya wabunge,"
amesema Kolimba
Awali wabunge tisa kutoka nchi sita wanachama wa EAC ambazo ni Kenya,
Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini waliapa kuwa wabunge
katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa bunge la Tanzania, Azzan Musa Zungu
amemwakilisha Spika wa Bunge, Job Ndugai pia walikuwepo Spika wa bunge
la Senate la Kenya, Ken Lusaka .Spika wabunge la Senate ya Rwanda,
Banard Mukuza, Spika wa bunge la Sudani Kusini, Anthony Makana.
Uganda yaiwekea ngumu Tanzania ubunge EALA
Reviewed by Unknown
on
December 18, 2017
Rating: 5
No comments:
Post a Comment