Trending News>>

Mvua yasababisha hasara jijini Mwanza

Mvua kubwa iliyonyesha kwa robo saa jijini Mwanza imezua taharuki na kuwaacha hasara wafanyabiashara baada ya bidhaa zao kusombwa na maji.

Wakati baadhi ya wafanyabisahara wakishangaa maji yalipotokea ikilinganishwa na muda iliyonyesha mvua hiyo, watembea kwa miguu, hasa eneo la Makoroboi wamekumbana na kero ya kukwepa madimbwi ya maji.

Mkazi wa Igogo, Bashiri Ntulua amesema mvua hiyo iliyonyesha leo Desemba 18, imemtia hasara kwa kutokana viatu vya wateja wake kusombwa na maji, huku vingine vikiloana na kumpa wakati mgumu wa kujitetea pindi wateja wake watakapokwenda kuchukua bidhaa zao.

Diana Mtovelo mkazi wa Nyamanoro amesema bidhaa alizokuwa amenunua kwa ajili ya kupeleka sokoni zimesombwa na maji.

"Naziomba mamlaka husika kuhakikisha zinaboresha  miundombinu hususani ya barabara za mijini ili kuepusha kutuama kwa maji wakati wa mvua," amesema Ripota wetu.

No comments:

Powered by Blogger.