Rose Muhando atema cheche kwa wanaomkebehi baada ya kujiunga CCM
Msanii
wa muziki wa Injili nchini Tanzania, Rose Muhando ameamua kufunguka ya
moyoni baada ya kupokea maoni mengi ya watu wakimponda kuhusu maamuzi
yake ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi.
Rose
Muhando amesema wanaomponda na kumkebehi anawachukulia ni watu wa
kawaida kwani hawezi kujifunza kwa watu walioshindwa huku akidai
ameshazoea kusemwa.
“Watu
wengine hawaelewagi nini wanachoongea, wanaongea ili waonekane nao
wanaongea. Mimi ni mtu ambaye ninayejitambua sawa eehhh!! mimi hata
sijali, nimeshazoea kutukanwa kwahiyo hata sihangaikagi na maneno yao.
"Mimi
ni funzi kwa walioshindwa na nimeondoka kwa walioshinda, walioshindwa
wana maneno mengi kutokana na nilishaimba uoga wako ndio umasikini wako,
Mimi siwezi kuishi kwa uoga kwenye nchi yangu kwani ni maamuzi yangu na
sijavunja sheria ya nchi na ningeogopa zaidi kama ingekuwa ni
dhambi.”amesema Rose Muhando kwenye mahojiano yake na E-Gospel ya Radio
E-FM.
Mapema
mwezi huu kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma, Rose
Muhando alialikwa kutumbuiza kwenye mkutano huo na kabla ya
kukaribishwa Jukwaani, Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema
Rose na Kundi lake wamekuja na maombi mawili likiwemo la kujiunga CCM na
kutumbuiza huku akisema kuwa vyote vimekubaliwa.
Awali
Rose Muhando hakuwa kwenye upande wowote wa vyama vya kisiasa na
amesema kujiunga CCM au Chama chochote ni maamuzi yake na sio dhambi
wala kosa kisheria.
No comments:
Post a Comment