Trending News>>

Msagasumu Vs Man Fongo, Pembeni Gigy Money… Hapatoshi Dar Live Leo!

Gigy Money.
DARR-RRR eeee salaa-aam! Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa pande zote za jiji na viunga vyake, hatimaye imefika ambapo leo katika kusherehekea Sikukuu ya Krismasi (Desemba, 25), Mfalme wa Singeli, Msaga Sumu, Man Fongo na wengine kibao watalishambulia jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live lililopo Mbagala-Zakhem ambapo patakuwa hapatoshi kwani mperampera utakuwa mpaka jogoo aseme kokolikooo!
ITAKUWAJE HII?
Jibu ni rahisi tu! Mapema kabla ya shoo hiyo ya kishindo, kutakuwa na burudani ya watoto ambayo itanogeshwa na Kundi la Wakali Dancers ambao ni wakali katika kucheza michezo kibao ikiwemo sarakasi.
Akichonga na Over Ze Weekend, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, wamewaandalia watoto michezo kibao ikiwemo kubembea, kupanda ndege spesho na kuteleza.
“Ni wakati wa wazazi kuwaachia watoto wote kuja kushiriki sikukuu hii maalum kwao. Tumehakikisha kila mtoto atakayekuja ataondoka na sapraiz ya aina  yake,” alisema KP na kuongeza:
“Tutakuwa na mashindano ya kuimba kwa watoto ambayo yataendeshwa na MC Darada huku mtoto atakayependeza kuliko wote atapatiwa zawadi spesho.
“Katika burudani hii ya watoto, pazia litafunguliwa mapema kuanzia 2:00 asubuhi huku kiingilio kikiwa kidogo kwa kila mzazi kuweza kumlipia mtoto wake ambayo ni shilingi 2,000 tu,” alisema KP.
WAKUBWA SASA!
KP alisema kuwa, burudani ya kibabe itakuwa mapema kuanzia saa 2:00 usiku huku kila kitu kikiwa kimeshapangwa kwenye mstari.
“Tukimaliza tu burudani ya watoto hiyo saa 12:00 jioni, kitakachofuata ni burudani ya kibabe hadi kuche.”
Gigy Money.
GIGY MONEY  KUPELEKA PAPA
Kwa mara ya kwanza tangu aingie kwenye Bongo Fleva, mkali ambaye pia ni video queen, Gigy Money atapeleka kihama ndani ya Dar Live kwa kugonga ngoma zake zote kuanzia Majojorijo hadi Papa.
“Ukisikia mashabiki kuimba Papa ndiyo leo. Andaa koromeo lako tu, kwa mara ya kwanza Papa itaimbwa na Gigy Money kwa kushirikiana na mashabiki wake,” alisema KP.
Man Fongo.
MAN FONGO NDANI
Naye mkali wa Singeli, Man Fongo atakusanya kijiji kama kawaida yake kwa kuwapigia ngoma kibao zikiwemo Siyo Poa na Hainaga Ushemeji.
“Tukizungumzia Singeli, basi Dar Live yote itakuwa ikinukia Singeli usiku huu. Ile Ngoma ya Hainaga Ushemeji ambayo ni ngoma ya taifa kwa mara nyingine itakuwa gumzo huku Man Fongo akiwaambia mashabiki wake wengine wasimchukulie poa yaani Siyo Poa.”
Msaga Sumu.
MSAGA SUMU
Mfalme wa Singeli, Msaga, kwa mara ya kwanza ataizima Dar Live kwa muda na kuwasha moto wenye rangi za kijani na nyekundu kwa kuwagongea ngoma zake zote zinazobamba kuanzia Naipenda Simba, Unanitega Shemeji hadi wimbo wa taifa ambao ni Mwanaume Mashine.
“Mashabiki wamesubiri kwa muda mrefu Albam ya Mwanaume Mashine, lakini jibu lao, leo ndiyo leo. Msaga Sumu ataifumua albam yote ya Mwanaume Mashine na niwaambie tu, watakao bahatika kufika, nadhani watawasimulia wenzao kwani zitapigwa kwanja zote za ndani ya albam hiyo ikiwemo ngoma yenyewe ya Mwanaume Mashine.”
WASINDIKIZAJI SASA!
Ili kunogesha shoo nzima, KP anasema kuwa shoo nzima itaongozwa na kundi kongwe la Muziki wa Taarab nchini la Jahazi Modern chini ya Prince Amigo, Asali Kiuno, Kidoti na mkali anayebamba na Ngoma ya Vidudu Washa, Pretty Kind ambapo kwa mara ya kwanza atalisimamisha jukwaa na madansa wake.
MTONYO JE?
Mbona simpo hiyooo! Shoo nzima ya kibabe utaipata kwa mtonyo mdogo sana yaani buku tano (shilingi 5,000 tu) na kwa wale 2000 watakaoingia mapema, kila mmoja atapatiwa ofa mkononi mwake ambayo ni sapraiz.

No comments:

Powered by Blogger.