Dr. Shein: Wala Rushwa CCM Wajadiliwe, Watimuliwe
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa chama kutosita kuwajadili
wanachama ambao wanakiuka maadili ya chama hususan vitendo vya rushwa.
Pia,
amesema wanachama hao wakishajadiliwa hawatasita kufukuzwa ndani ya CCM
na kwamba imefikia hatua baadhi ya watu hao ambao wanafanya vitendo
hivyo wanaonewa haya.
Hayo
ameyasema jana , katika sherehe za kumpongeza kuchaguliwa tena nafasi
ya Makamu Mwenyekiti, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa
Mjini ,ambapo aliwataka viongozi hao kutofumbia macho vitendo hivyo
ndani ya CCM.
Katika
maongezi yake Dk.Shein aliongeza kuwa vitendo hivyo vya rushwa si jambo
jipya ndani ya CCM na kwamba inaharibu sana maadili ya chama.
“Vitendo
hivi vya rushwa ndani ya CCM si suala jipya lakini tunaoneana huruma,
tunafichiana na baadae tunalalamikiana wakati chama ni ya wanachama
hivyo lazima tushirikiane,”alisema.
Makamu
Mwenyekiti huyo Dk.Shein alisema utaratibu wa chama kinajielekeza
wanachama ambao wanakiuka maadili wanapaswa kujadiliwa kuanzia ngazi za
tawi na baadae inawasilishwa kwenye uongozi wa juu na kuchukuliwa hatua.
Alieleza
chama kipo kwa wanachama ikiwemo kwenye mashina na matawi na taratibu
zinafafanua kuwa ngazi hizo ndipo mambo hayo yanazungumzwa kwamba
mwanachama akikiuka maadili anajadiliwa kwenye tawi.
“Anajadiliwa
kwenye kamati ya tawi na shina, kamati ya jimbo, kamati ya wilaya,
Halmashauri ya wilaya ndipo wanapojadiliwa huku kwamba anafaa ama hafai
hachukuliwe hatua za kufukuzwa ama asichukuliwe,”alisema.
Makamu
Mwenyekiti huyo alisema utaratibu unaeleza kuwa baada ya kujadiliwa
wanachama hao taarifa itapelekwa kwenye ngazi za juu na kufanya maamuzi
ya kumfukuza.
“Nachotaka
kueleza kuwa kazi hii ni ya wote na kwamba jukumu kubwa ni kuhakikisha
CCM inashinda mwaka 2020 msiwafiche watu ambao wanataka kuharibu chama,
na kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwa ndumi la kuhili tunayoyasema sio
tunayoyafanya,”alisema Makamu Mwenyekiti.
Alifafanua
kuwa kazi ya siasa ya kipindi hiki lazima kuongeza kasi ambapo kuna
mambo zaidi ya kuyafanya na hata Mwenyekiti Dk.John Magufuli alisisitiza
kwenye mkutano mkuu uliofanyika Desemba 18, mwaka huu mjini Dodoma.
Mbali
na hilo, Dk.Shein aliwataka viongozi wa serikali kutambua na kuheshimu
CCM kutokana na kuwa wanafanya kazi ya utekelezaji wa chama hivyo
hawanabudi kukithamni.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Dk.Abdallah Juma
Saadalla(Mabodi), alisema wanachama kutoka visiwani humo wanatarajia
kusimamia vyema ibara ya tano ya kuhakikisha CCM inashinda mwaka 2020.
Aliongeza kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na mawimbi makubwa sana lakini watu walioshiriki walikuwa wanastahili.
“Bado
tunafanya juhudi za kutoa elimu kwa viongozi wa chama kuhusu suala la
kuzingatia kanuni na maadili ili kuhakikisha wanasongesha gurudu la
uchaguzi wa mwaka 2020″alisema.
Dk.Mabodi
ameeleza kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa wagombea wote ambao wamepita
kwenye uchaguzi huo asilimia kubwa wana maadili ya kutosha.
No comments:
Post a Comment