Muuza Bangi Aingia Kimakosa Ndani ya Gari la Polisi Akidhani ni Teksi
MTU
mmoja anayedaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya amejikuta
akipata wakati mgumu katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismasi baada
ya kuingia kwenye teksi akiwa na misokoto takribani 1000 ya bangi pasipo
kufahamu kuwa anaingia kwenye gari la polisi.
Tukio
hilo la aina yake limetokea hivi karibuni katika eneo la Christiana, Mji
Mkuu wa Copenhagen maarufu kwa biashara ya madawa ya kulevya nchini
Denmark ambapo inasemekana mwanamume huyo alikuwa akirudi nyumbani
kutoka kwenye biashara zake hizo haramu.
Polisi
wameeleza kufurahishwa na ufanisi wa tukio hilo kwani mtuhumiwa huyo
walikuwa wakimsaka muda mrefu hivyo wamemfunguliwa mashtaka ya kuhusika
na biashsra ya madawa ya kulevya.
Nchini Denmark, biashara ya madawa ya
kulevya ni haramu na Wilaya ya Christiana miezi ya hivi karibuni msako
mkali ulifanyika kuwatafuta wauza madawa ya kulevya .
No comments:
Post a Comment