Marekani iko tayari kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini
Rex Tillerson
Marekani iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema.
Taaarifa yake ilionekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabala ya mazungummzo yoyote kufanyika
Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wake Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika.
Hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia imesababisha Marekani kuongoza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo.
Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel
Kando na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Korean Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la nchi za Atlantic siku ya Jumanne, Bw Tillerson alisema kuwa Marekani haiwezi kukubali Korea Kaskazini kujihami kwa silaha za nyuklia.
No comments:
Post a Comment