Klabu ya Galatasaray Yamuonea Huruma Eboue na Kumpa Dili Hili
Baada
ya nyota wa zamani wa Ivory Coast Emmanuel Eboue kupoteza fedha zake
kwa mke wake wa zamani hatimaye klabu ya Galatasaray ya Uturuki imempa
nafasi ya kuwa kocha.
Eboue
ambaye amewahi kutamba na klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Arsenal
amepewa nafasi ya kuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana chini ya umri
wa miaka 14 (U-14) ya klabu ya Galatasaray.
Galatasaray
imemtaka Eboue kushughulikia leseni yake ya kufundisha soka ili aweze
kuanza kibarua rasmi ndani ya timu hiyo ili kuokoa hali yake ya
kimaisha.
Klabu
hiyo inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu soka ya
Uturuki, imemwahidi mshahara mnono ili kusaidia kurejesha hali yake
nzuri ya kimaisha.
Eboue
amejikuta kwenye wakati mgumu wa maisha baada ya mahakama kuamuru mali
zote kukabidhi kwa mke wake. Eboue na mke wake waliachana huku akiwa
ameandika jina la mkewe katika sehemu kubwa ya mali zake ikiwemo nyumba
za kifahari alizokuwa amezinunua kutokana na malipo yake kama mchezaji.
No comments:
Post a Comment