Harmorapa Akiri Kwenda Kwa Mganga wa Kienyeji Kisa Penzi la Wema Sepetu
Msanii
wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kusema kuwa katika
mwaka 2017 amehangaika kulipata penzi la mwanadada Wema Sepetu kiasi cha
kuamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mara tatu ili aweze kumpata mrembo
huyo.
Harmorapa
akiongea kwenye kipindi cha eNewz cha EATV amedai kuwa baada ya
kuhangaika kwa marafiki zake Wema Sepetu na kugonga mwamba aliamua
kwenda kwa babu (mganga) ambapo amedai kwa mara ya kwanza aliambiwa
apeleke kuku mweupe, na alipeleka huyo kuku lakini aliporudi mjini Dar
es Salaam mambo yake yakawa bado vile vile.
"Nimemuendea
kwa babu Wema Sepetu mara tatu, nilipokwenda mara ya kwanza niliambiwa
nipeleke kuku mweupe, nikapeleka zangu yule kuku mganga akafanya yake
lakini niliporudi mjini sikuona mabadiliko yoyote yale, nikamfuata tena
babu akaniambia nipeleke vitu vingine viwili ambavyo hapa nashindwa
kuvisema" alisema Harmorapa
Harmorapa
aliendelea kufunguka jinsi ambavyo amehangaika kulitafuta penzi la
Wema Sepetu na kudai ilifika wakati aliambiwa apeleke mchanga wa unyayo
wa Wema Sepetu au mchanga ambao mwanadada huyo ametemea mate, kitu
ambacho Harmorapa amedai kilikuwa kigumu sana kwake kwa sababu hapati
nafasi ya kukutana live na Wema Sepetu.
Hata
hivyo Harmorapa kwa sasa amesema amemwachia Mungu juu ya jambo hilo
baada ya kuona harakati za kwa mganga wa kienyeji zinakwama.
No comments:
Post a Comment