Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Kutembelewa na Mwenyekiti Mpya wa BAVICHA
Mbunge
wa Singida Mashariki ambaye sasa Kenya akiendelea na matibabu kufuatia
kupigwa risasi Septemba 7, 2017 amefunguka juu ya viongozi ambao
wanasaliti CHADEMA na kusema jambo hilo lisiwatishe bali wao waendelee
na kazi yao.
Tundu
Lissu aliyasema hayo jana alipoonana Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Patrick Ole Sosopi ambaye alimtembelea Mhe
Lissu hospitali jijini Nairobi jana kumjulia hali
"Ndugu
zangu Mhe Lissu ameweza kunieleza mambo mengi sana na binafsi naamini
ameniagiza kwa niaba ya Baraza la Vijana na tutayetekeleza kwa maslahi
mapana ya nchi na chama chetu, hajasita kuniambia kwamba hali ya siasa
yetu ndani ya nchi yetu kwa biashara inayoendelea kununua Viongozi
uchwara na wenye tamaa wa chama chetu, amesema tusipate hofu CHADEMA
hatujaanza kusalitiwa leo na hao wanaondoka, sio ajabu hata kidogo kwani
mbona Yesu aliwahi kusalitiwa tena na mwanafunzi wake na hakuacha kazi
yake" aliandika Ole Sosopi
Aidha
Sosopi aliendelea kusema kuwa Tundu Lissu amemweleza kuwa hata watu
ambao waliwahi kuisaliti CHADEMA kipindi cha nyuma hawajapata mafanikio
yoyote katika maisha yao
"Wanaotusaliti
hawajawahi kuwa na mafanikio katika maisha yao, tusikate tamaa
mapambano yaendelee. Mwisho kabisa Mhe. Lissu ametuma salamu nyingi kwa
Watanzania wote wanaoendelea Kumchangia na Kumuombea, ameendelea
kuwasihi waendelee kumchangia na kumuombea, maana Bunge na serikali
wamekataa kabisa kumtibia ili hali kwa mujibu wa sheria ni haki yake"
alisema Ole Sosopi
No comments:
Post a Comment