MICHEZO:Masau Bwire anahisi aibu kutaja jina la Ammy Ninje
Afisa habari wa Ruvu Shooting ya ligi kuu Tanzania bara Masau
Bwire amesema anahisi aibu kulitamka jina la kocha wa timu ya
Kilimanjaro Stars Ammy Ninje kwa sababu ndio amelisikia kwa mara ya
kwanza baada ya kocha huyo kupewa jukumu la kuifundisha timu hiyo kwenye
michuano ya CECAFA Challenge Cup 2017.
Bwire amesema, jina hilo ni geni kwake na hakuwahi kulisikia kabla ya kocha huyo kupewa majukumu ya kuifundisha Kili Stars, kutokana na matokeo mabaya ya kikosi cha Kili Stars kwenye michuano ya Chalenji, Bwire amehoji uwezo wa Ammy Ninje.
“Mwalimu kwanza nilikuwa simjui hili jina ndio mara ya kwanza nalisikia, hata kulitamka naona aibu, ametokea wapi amefundisha wapi, ana sifa zipi, hatujui. Labda kama wapo watanzania wengine ambao wanalifahamu hili jina kwa ufasaha sana na wameshuhudia amefundisha wapi na hiyo timu ikawa na mafanikio gani labda waseme.”
“Hatujui alikoibukia, uteuzi na uchaguzi wa walimu wa kufundisha timu ya taifa pia uangaliwe. Tusichukuwe mtu ambaye anakuja na maneno mengi kiingereza kingi tukaona kwamba huyu msomi anajua mambo kwa sababu mnaweza mkaongea na mtu anachomekachomeka visheria vya mpira ukaona huyu ndio anafaa.”
“Tuwapambanishe, hawa tulionao hapa hawawezi? Kwa sababu huwezi kumchukua kocha ambaye watanzania wengi hawamjui, ukipita huko mtaani wengine hata kulitamka hawajui.”

No comments:
Post a Comment