Kanusho la taarifa inayosambazwa kumuhusu Makamu wa Rais
Ofisi
ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo
linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa
atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya
tarehe 1-1-2018.
Ofisi
ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la
kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho
kwa tarehe iliyotajwa.
Ikumbukwe
kuwa siku ya tarehe 15-12-2017 wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu
ya Nchi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo
itaratibiwa na Ofisi yake .
Ofisi
ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia matangazo, taarifa na
ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya upandaji miti
Dodoma.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma
30 Desemba, 2017.
No comments:
Post a Comment