Trending News>>

El Clasico kuisimamisha dunia kwa dakika 90, ni Madrid au Barcelona hii leo?

Dunia inasimama kwa dakika 90 hii leo kupisha pambano kubwa zaidi la vilabu hapa duniani litakalopigwa leo pale Hispania, ndio ni El Clasico mchezo ambao kila mpenda soka lazima afuatilie.
Pambano la leo lina mambo mengi yanayolifanya liwe na utamu sana kwani achana na masuala ya siasa za Catalunya na Hispania, mchezo wa leo unaweza kuwatoa kabisa Madrid katika mbio za ubingwa au kuwarudisha.
Pamoja na kwamba Barcelona wameshawaacha Real Madrid kwa alama 11 hadi sasa katika ligi kuu La Liga lakini El Clasico ni tofauti sana kwani hakuna timu ambayo inaonekana rahisi siku hii.
Kwa mwaka huu Real Madrid wanaonekana wababe wa El Clasico kwani wameshashinda mbili zilizopita 2017 na kama wakishinda ya leo watakuwa wameshinda 3 mfululizo kama walivyofanya mwaka 1978.
Patrick O’Connel mwaka 1940 alikuwa kocha wa kwanza kupoteza michezo yake mitatu ya mwanzo ya El Clasico na kama Ernesto Valverde atakubali kufungwa hii leo baasi atafuata nyayo za O’Connel.
Wakati Valverde akitafutwa na rekodi mbaya ya kupigwa mara 3 mfululizo,Zinedine Zidane yeye kwa upande wake atakuwa anatafuta rekodi iliyowekwa na Alfredo Di Stefano ya kushinda El Clasico 3 mfululizo.
Cristiano Ronaldo anaonekana mfalme wa michezo hii kwani hadi sasa amefunga mabao 17 katika mchezo huu wa El Clasico na kama atafanikiwa kufunga bao moja katika mchezo atafikia rekodi ya Di Stefanio mwenye mabao 18 katika El Clasico.
Wakati Cristiano Ronaldo akitafuta rekodi hiyo ya Di Steafanio, Lioneil Messi anakwenda katika mchezo huu akiwa mfalme wa mabao ambapo hadi sasa ana mabao 24 katika El Clasico zote huku 4 akiyafunga Santiago Bernabeu.
Azam Tv watakuletea mchezo huu hadi sebuleni kwako kutokea pale Santiago Bernabeu ambapo utapata kujua kama Barcelona watakubali kuendelea kuwa vibonde wa Madrid au Valverde anakatiza utemi wa Zidane.

No comments:

Powered by Blogger.