Kisa Kuolewa Na Serengeti Boy… Mama Mobeto Amchana Mama Esma
MAMA mzazi wa Mwanamitindo maarufu Bongo Hamisa Mobeto, Shufaa
Lutigunga amefunguka kuwa hayuko tayari kuolewa na “Serengeti Boy”
wakati watu wazima wenzie wapo, kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa ni
kumchana mama Esma.
Akizungumza na Risasi Jumamosi Mama Mobeto alisema kuwa, sasa hivi
ameshakuwa mtu mzima na ni bibi mwenye wajukuu hivyo kuolewa na kijana
mdogo ni kujishushia hadhi kama mama na bibi pia.
“Jamani mimi kama ni kuolewa basi nitaolewa na mtu mzima mwenzangu
kwasababu Serengeti Boy kwangu haiwezekani, nahitaji kuolewa kweli ila
nitaolewa na mzee mwenzangu ili wajukuu wapate babu,” alisema Mama
Mobeto ambaye kwa kuongea hayo ni kama amemchana mama Esma amefunga ndoa
hivi karibuni na kijana anayedaiwa kuwa ni Serengeti Boy kwake
No comments:
Post a Comment