Trending News>>

Basi la Abiria Likiendeshwa na Kijana wa Miaka 16 Latumbukia Mtoni na Kuua 32

Basi lililokua na abiria 50 nchini India limeanguka katika daraja moja na kuwaua takriban watu 32 lilipoingia katika maji Kaskazini mwa India kwa mujibu wa polisi.
Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na kijana wa miaka 16 lilipoteza mwelekeo kabla ya kuanguka mita 30 katika mto Banas. Lilikuwa likiwabeba abiria kutoka eneo la Rajasthan kuelekea Ramdevji katika wilaya ya Sawai Madhopur kulingana na vyombo vya habari.


Polisi waliohojiwa na jarida la Hindustan wanasema kuwa dereva huyo ni miongoni mwa wale waliofariki likimtaja kuwa mtoto asiye na mafunzo ya udereva.
Wengi wa waathirika , ikiwemo wanawake na watoto walikufa maji kulingana na mamlaka. Huduma za uokoaji zililazimika kukata mabaki ya basi hilo lili kuwaokoa manusura ambalo lilikuwa limezikwa chini ya daraja hilo. Basi hilo baadaye lilivutwa nje ya mto huo.

No comments:

Powered by Blogger.