Daladala kutumika kusafirisha abiria Mikoani
Dar es salaam. Magari ya abiria (daladala) yameanza kutumika kupakia abiria wanaosafiri kwenda mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kupunguza adha ya usafiri kwa abiria wanaosafiri msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Akizungumza na Mwananchi, leo Jumanne Desemba 19, Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT),Inspekta Swamix Ibrahimu amesema gari hizo zimeanza kubeba abiria na asubuhi ya leo daladala nne zimeondoka kuelekea Moshi na Arusha.
"Daladala unazoziona hapa, tunazikagua na zipo kwaajili ya dharura endapo itatokea abiria wakawa wengi basi tunaruhusu zinapakia "amesema.
Si kwamba zinapakia muda wowote, hapana tutakuwa na daladala tano kwa siku ambazo zinakuwepo ikitokea abiria wameongezeka na basi kubwa hakuna basi tunaruhusu" amesema
Ibrahimu amesema abiria bado hawajawa wengi kiasi cha kuruhusu daladala nyingi kupakia. Mmoja wa wasimamizi wa daladala ambazo zimekutwa zikikaguliwa, Ignas Swai amesema gari zake ni imara na tayari zimekaguliwa na Askari na kupewa kibali na Sumatra.
"Nauli tunatumia IleIle iliyowekwa na Sumatra na tunapakia abiria wanaoenda Moshi na Arusha "amesema.
No comments:
Post a Comment