Jinsi “soda” ilivyomkomaza Gabriel Jesus na sababu ya ushangiliaji wake wa simu
Chupa ya Champagne ni ghali sana kwa kijana ambaye amezaliwa
mtaani na hana uhakika kuhusu maisha, kwa kijana ambaye amesota sana
katika mitaa ya Sao Paulo kama Gabriel Jesus hakika Champagne ndio
ingekuwa bata yake.
Lakini Jesus amesema hapana Champagne sio kitu kama soda walizokuwa wakigombea mjini Sao Paulo na kusema kwamba soda hizo japo ni bei rahisi sana nchini kwao lakini ni tamu mara 10 kuliko mivinyo hiyo.
Unajua nini kimezifanya kuwa tamu soda hizo? Ni jinsi zilivyopatikana kwani Jesus anasema ilibidi utumie jasho jingi,machozi hata na damu wakati mwingine ili kupata chupa hiyo ya soda na ilikuwa fahari kwao.
Jesus anasema kulikuwa na mashindano ya mtaani ambayo yalichezwa katika viwanja vibovu na wakati mwingne barabarani na timu zilikuwa ngumu sana lakini mshindi wa mashindano hayo anapata soda.
Hilo lilimkomaza sana Jesus kisoka kwani alijituma sana yeye pamoja na wenzake kupata soda hizo na anakiri kwamba pale walipokuwa wakishinda walizunguka na soda hizo mtaa mzima wakiwaonesha watu ushindi wao.
Gabriel Jesus anasema akiwa na miaka 13 tu alianza kucheza na watu wakubwa ambao walikuwa wakimchezea rafu za makusudi na muda mwingine kumpiga kutokana na chenga zake na soka la maudhi.
Jesus hatasahau siku ambayo alikoswa na rafu mbaya na mtu aliyekuwa mkubwa kwake na baada ya mtu yule kumkosa Jesus aliamua kwenda nje ya uwanja ili amsubiri Jesus ampige kutokana na kumpiga Chenga lakini Jesus anashukuru rafiki zake walimuokoa.
Gabriel anaamini mji wa Sao Paulo ulichangia sana yeye kukomaa kisoka na alipokwenda Man City aliogopa sana na kuhisi anaweza kupoteza kila kitu kwani hakuwa anajua sehemu nyingine zaidi ya Sao Paulo.
Jesus anasema maisha ya Manchester yalikuwa ya upweke sana kwani alikuwa hamuoni mama yake wala marafiki zake na hii ikamfanya awe mpweke sana hali ambayo baadae alianza kuizoea.
Kuhusu ushangiliaji wake Jesus anasema huwa ana kaka yake ambaye kila akifunga goli humpigia simu pale mpira unapoingia tu nyavuni na ndio maana huweka vidole sikioni ishara ya kupokea simu ya kaka yake.
Tangu ajiunge City Jesus amefunga mabao 17 katika michezo 35, akifunga mabao 21 katika michezo 48 aliyoichezea Palmeiras huku akiifungia timu ya taifa ya Brazil mabao 8 katika michezo 13 aliyowachezea.

No comments:
Post a Comment