Dakika 5 mabao 3, Arsenal waishangaza Liverpool Emirates
Ilikuwa usiku mbaya kwa vijana wa Arsene Wenger baada ya
Arsenal kwa mara ya kwanza kumaliza kipindi cha kwanza bila kupiga shuti
langoni mwa wapinzani tangu mwezi January.
Bao la Phellipe Coutinho dakika ya 26 la mchezo liliifanya Liverpool
kuwa klabu ya 4 kufunga mabao 700+ baada ya Manchester United(840),
Arsenal(744) na Chelsea(709), .
Baada
ya kipindi cha kwanza kuisha ilionekana kama Arsenal wanakufa katika
mchezo huo lakini filamu ilianza katika kipindi cha pili ambapo mabao 5
yalifungwa.
Mo Salah aliwapa matumaini mashabiki wa Liverpool akifunga bao la
pili na likiwa la 15 kwake msimu huu lakini Alexis Sanchez dakika ya 53
alifufua matumaini ya Arsenal.
Dakika 3 baadae kiungo wa Arsenal Granit Xhaka aliipatia Gunners bao
la kusawazisha kabla ya Mesut dakila ya 58 kuiandikia Arsenal bao la 3,
dakika ya 71 Roberto Firminho aliufanya mchezo kuwa tatu tatu.
Kwa mabao yaliyofungwa leo yanaifanya Liverpool kuwa timu inayoongoza
kwa mabao ya ugenini katika ligi kuu kubwa 5 barani Ulaya wakiwa
wamefunga mabao 27 katika mechi 10.
No comments:
Post a Comment