Mapipa 200 ya kemikali yakamatwa Mwanza
Mamlaka
ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama imekamata mapipa 200 sawa na lita
za ujazo 50,000 ya shehena ya kemikali bashirifu idhaniwayo kuwa ni
ethyl alcohol.
Taarifa
iliyotolewa na Kamishina wa Ukaguzi na Sayansi Jinai, DCEA, Bertha
Mamuya jana Desemba 22 inaeleza kuwa kiasi hicho kilikamatwa Desemba 13
mwaka huu katika kivuko cha Kigongo wilayani Misungwi.
Alisema
kemikali hiyo ilikuwa ikisafirishwa na kampuni ya Mwanza Lake Line
Industiries kwenda mjini Kinshasa nchini DRC Congo, ikiwa kwenye gari
linalomilikiwa na kampuni ya Mhili ya jijini Mwanza.
“Gari hili lilikamatwa likiwa halina nyaraka zinazoruhusu kisheria kusafirisha kemikali hizo,” alisema na kuongeza,
“Kitendo
hicho ni ukiukwaji wa sheria namba tatu ya kemikali za viwanda na
nyumbani ya mwaka 2003, na sheria ya dawa za kulevya namba tano ya mwaka
2015 na marekebisho yake ya mwaka 2017.”
Alisema
kampuni hiyo ya Lake Line ikiwa inatambua kuwa imekiuka utaratibu za
kujihusisha na kemikali, Desemba 14, iliidanganya mamlaka ya Mkemia Mkuu
wa Serikali kwa kuomba kibali cha kutaka kusafirisha kemikali bashirifu
na kupewa kibali hicho wakati tayari gari lenye kemikali hizo lilikuwa
limeshakamatwa.
Alisema
uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kampuni hiyo imewasilisha taarifa
za uongo katika mamlaka mbalimbali za udhibiti, ikiwamo kiasi cha
kemikali kilichokuwa kinasafirishwa na magari yaliyotakiwa kuisafirisha.
Alisema
DCEA kwa kushirikiana na mamlaka nyingine inaendelea kufanya uchunguzi
zaidi kuhusu kampuni hiyo na kwamba uchunguzi utakapokamilika, hatua
zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika.
No comments:
Post a Comment