CR7 pamoja na kocha wake, ligi yake, timu yake na wakala wake waziteka tuzo za Global
Huu ni mwaka wa neema kwa Mreno Cristiano Ronaldo kwani
pamoja na kwamba Real Madrid hawafanyi vizuri lakini haikumzuia kubeba
tuzo ya mwanasoka bora wa dunia tuzo za Dubai Global Soccer.
Wakati
CR7 akibeba tuzo hiyo, ligi anayoshiriki Cristiano Ronaldo ya La Liga
imezibwaga ligi za EPL, Serie A na Bundesliga kwa kuibuka kama ligi bora
zaidi kwa mwaka 2017 huku timu ya CR7 Real Madrid wakiibuka kuwa timu
bora 2017.
Kocha
wa Real Madrid Zinedine Zidane ambaye pia ni kocha wa Ronaldo alitwaa
tuzo ya kocha bora huku wakala wa Ronaldo Jeorge Mendez akiibuka kidedea
kama wakala bora wa kwa mara ya saba wachezaji kwa mwaka 2017.
Gwiji
wa zamani wa Italia Fransesco Totti alitwaa tuzo ya heshima kwa
wachezaji huku kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Marcelo Lippi
akitwaa tuzo ya heshima kwa upande wa makocha.
Tuzo
ya kocha bora imeenda kwa kocha wa nchini Ujerumani Felix Brych huku
Hector Cuper baada ya kuisaidia Misri kwenda katika fainali za kombe la
dunia amepewa tuzo ya kocha bora wa nchi za kiarabu.
No comments:
Post a Comment