Coutinho Barcelona, Dyabala Manchester United, hizi hapa tetesi za usajili
Add caption |
Tayari beki wa Liverpool Virgil Van Djik ameshaaga mashabiki
wa klabu ya Southampton tayari kuelekea kuwatumikia majogoo wa London
Liverpool kwa ajili ya msimu ujao wa EPL.
Wakati mashabiki wa Liverpool wakifurahia Van Djik kusaini Liverpool
kuna habari mbaya kuhusu wao, habari mbaya ni kwamba Barcelona wametuma
wawakilishi wao kwa ajili ya kukutana na Phelipe Coutinho tarehe 3 ili
kuangalia namna ya kumnunua.
Ukiachana na Liverpool habari nyingine ya usajili nchini Uingereza
inazihusu vilabu vya Manchester(United na City) ambao wote wanatajwa
kujiandaa kutoa £50m kuishawishi Barcelona kwa ajili ya Samuel Umtiti.
Baada ya kulalamika kwamba hawajatumia sana pesa katika usajili sasa
kocha wa Manchester United Jose Mourinho anajiandaa kutuma kiasi cha
£60m kwa klabu ya Juventus ili kumnunua Muargentina Paulo Dyabala.
Kocha wa klabi ya Everton Sam Allatdayce ameamua kuongeza nguvu ya
ushambuliaji katika kikosi chake baada ya kocha huyo kukukaribia
kumnunua mshambuliaji wa Bestikas Cenk Tosun huku pia Steven Nzonzi
akiwa katika rada za Big Sam.
Klabu ya Juventus imeripotiwa kukataa kiasi cha pesa £35m ambazo
Arsenal wanadaiwa kutuma kwa ajili ya kutaka kumnunua mlinzi Medhi
Benatia na sasa Juve wamewataka Arsenal kuongeza kiasi hicho cha pesa.
No comments:
Post a Comment