Waziri Mkuu apokea wanachama 60 wa CUF
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 60 kutoka Chama cha
Wananchi (CUF) ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wanachama
hao wamepokelewa Desemba 29, 2017 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye kijiji cha Nkowe kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Kabla
ya kuwakabidhi kadi za CCM, Waziri Mkuu alipokea kadi za CUF kutoka kwa
vijana saba kwa niaba ya wenzao 60. Vijana hao ni Hamisi Juma, Fatuma
Abdallah, Mwajuma Mohammed, Thomas Moto, Zainab Nachiluku, Samia Said na
Juma Said.
Vijana hao saba waliokabidhiwa kadi mpya za CCM pamoja na wenzao 53, walikula kiapo cha uaminifu.
Kwa
mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama
wote ni vijana ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali na
wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano.
Bw. Essau alisema wanachama hao wote wametoka vijiji vya Kipindimbi, Nkowe na Mpumbe.
Novemba
5, mwaka huu, Waziri Mkuu alipokea wanachama 37 kutoka vyama vya CUF na
CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera,
wilayani Ruangwa.
No comments:
Post a Comment