Trending News>>

SIMULIZI :: Jini Mahabati Sehemu ya Ishirini na Nne (Kwa wenye miaka 18+)


fake
SIMULIZI : JINI MAHABATI
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
MTUNZI: MANYAMAJR:
AGE: 18+
ILIPOISHIA
Utaalamu huu ukaendelea mpaka ukafikia hatua ya kupandikiza mbegu nje ya tumbo la uzazi, zikapandikizwa ndani ya chupa iliyoandaliwa maalumu kwa kazi hiyo. Chupa hii huwa mithili ya kitaru cha miche ambapo ikikua huenda kupandikizwa shambani. Hivyo ndivyo ilivyo kwa chupa hii, baada ya muda fulani kupita tangu kupandikizwa kwa yai, yai hilo hurejeshwa tena katika tumbo la mwanamke lililotwaliwa kwake yai hilo au kwa mwanamke mwingine yeyote. Na pengine huwekwa katika tumbo la hayawani mwingine asiye mwanadamu ili aibebe mimba hiyo aliyopandikizwa badala ya binadamu (mwanamke).
Kwa hio una maanisha tunaweza kupandikiza hata kwa viumbe vingine kama wanayama na watoto bado wakazaliwa alihoji mmoja wa majini. “Kabisa hilo linawezekana na hata mkitaka tujaribu tutajaribu” Dr Maisoso alifafanua na kuongeza hapa ndipo ulipofumuka upinzani dhidi ya upandikizaji huu wa mimba kutoka katika majukwaa ya kidini na ya kisiasa. Khasa khasa pale upandikizaji unapowahusisha watu wasiokuwa mke na mume, au ulezi wa mimba anapopewa mwanamke mwingine au mnyama.
Sawa sawa Dokta tunakuelewa huo upinzani wa binadamu wakihusisha na vitabu vitakatifu vya dini sisi haituhusi maana sisi tunaamini katika imani ambazo hata hao binadamu hawawezijua” alitoa hoja mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.
Mjumbe mwingine akasimama na kuomba ufafanuzi kuhusu upandikizaji wa mbegu ambazo kitaalamu unaitwa In Vitro Fertilization (IVF). Hapo ikawa nafasi nzuri kwa kwa Daktari Maisoso kutoa tena ufafanuzi wa kitaalam. Dokta Maisoso anasema “yai la mama hupevushwa kwa kutumia dawa maalumu na hufuatiliwa kwa kutumia mashine ya uchunguzi wa ndani ya mwili(Ultrasound).
“Baada ya yai kukomaa, sindano maalum yenye wembamba mithili ya unywele huingizwa ukeni hadi kwenye mirija na yai lililopevuka huchukuliwa na kutolewa nje,” anasema. Yai au mayai hayo huwekwa kwenye chombo maalumu (test tube) kabla ya kuhamishwa kwenye beseni maalumu ambalo hufanya yai liendelee kuwa hai licha ya kutoka nje ya mwili wa binadamu. “Beseni hilo halina budi kuwa na mazingira kama ya mwilini. Kwa mfano joto, mwanga na kusiwepo na sauti, kwani yai huweza kuharibika kwa kasoro ndogo ndogo sana,” anasema.
Anasema wakati huo mbegu za mwanaume hupimwa kama hazina walakini na hutolewa kwa mwanaume kujichua au kama hawezi kujichua basi hutakiwa kufanya tendo la ndoa na mke wake na kisha mbegu kukingwa kabla ya kuwekwa kwenye chombo maalumu.
Mbegu za baba hutakiwa kutolewa saa mbili mara tu baada ya yai la mama kutolewa ili visipishane. “Baada ya yai na mbegu kutolewa, hatua inayofuata ni kuichoma mbegu kwenye yai kwa kutumia sindano maalumu. Mchakato huu unaitwa kwa kitaalamu, Intra Cytoplasmic Sperm Injection au ICSI),” anasema.Dokta huyo anaeleza kuwa, baada ya mbegu na yai kuchanganywa, huwekwa kwenye chombo maalumu cha joto kitaalamu ‘Incubator” kwa saa 40 kabla ya kuwekwa au kupandikizwa kwenye kizazi cha mama.
“Hali kadhalika ‘incubator’ inatakiwa kuiga hali ya tumboni mwa mama wakati yai la mama na mbegu za baba vinapowekwa kabla ya kuwekwa kwenye kizazi cha mama, kwa mfano joto, mwanga na sauti,” anasema DR Maisoso. Dr Maisoso IVF ina mafanikio makubwa kwa mtu au kiumbe yeyote isipokuwa wanawake wenye umri wa miaka 40 na kuendelea. Hapo dokta huyu jinni lenye utaalamu mkubwa likawa kama limeweka nukta na kuanza kusikilizia nini kitakuwa kinaendelea.
“Kama kuna mtu anaswalia anaruhusiwa kuuliza” alisema Dokta huyo na kukaa kimya. Watu wote walikuwa kimya wakiangaliana ni nani aulize swali. Akasima jinni mwingine na kuuliza kwa hiyo hizo maniiia ambazo jinni Barike anasema zipo za kutosha zimehifadhiwa wapi. Yule yule Dokta akasimama na kujibu swali hilo. Kwa sasa tuna benki yetu maalumu ya kuhifadhi manii hizo na kutokana na sayansi na teknolojia tuliyonayo pengine kuliko hata binadamu zinaweza kukaa kwa mda mrefu.
Baada ya majibu hayo na wahusika kukaa kimya dokta huyo akaamua kukaa chini na kuacha mambo mengine yaendeelee. Asante sana dakatari kwa ufafanuzi wako huo sasa tunaomba tujadili kuhusu habari za watu waliokuwa wakimfuatilia yule binti ambaye tulimridhia” alisema mwenyekiti wa kikao hicho.
Hapo jini Makata akasimama na kusema “Jamani ile kazi ya kumtoa uhai na kumwangamiza baba yake na Tariq imekuwa ngumu sana maana kwa sasa amekimbilia kwa mtaalamu wa majini. Ila pamoja na hayo bado tuliweza kumtumia popo mwenye mabawa ili aweze kumshkisha adabu. Si hivyo tu pa tumeweza kumtia ububu ili hasiweze kusema kitu chochote kwa mtaalamu huyo” alifafanua jini Makata na kukaa chini. “Kwa hiyo nini kinaendelea mpaka sasa aliuliza mwenyekiti wa kikao. “Kinachoendelea tunasubiri reaction ya huyo mtaalamu wa Zanzibar ili tuone atafanyaje ili kupambana na dhahama ambayo tumempa baba huyo. “Kweli kabisa sisi ni kukomaa tu na hiyo mbinu ya kumtia ububu.
Sawa kabisa hiyo ni mbinu bora na itafanikiwa lazima, alidakia jini mwingine. Basi kikao kikafungwa na jini Barike akaagizwa aendelee na majukumu yake ya kuhakikisha anawapelekea manii za kutosha kule kwenye benki maalumu iliyotengenezwa kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa hizo.
Wazo la mwisho lilikuwa ni kumtupia jinni la mkosi baba yake na Tariq ili iwe ngumu sana kwa huyo mtaalamu kujua anapambana na jinni lipi.
Baada ya baba yake na Tariq kuingiliwa na lile jini lenye mabawa na kumzalilisha na kumtaka aende mjini kutangaza uzalishaji huo mzee huyo aliamua kwenda kwa mtalamu wa majini huko Zanzibar. Alipofika tu akakumbwa na mkasa mwingine yaani alipigwa kombora cha kuwa bubu na kushindwa kuelezea nini kilitokea. Baada ya mtaalamu huyo wa viumbe hivyo kugundua kuwa mzee huyo alikuwa na bifu kubwa sana baina yake na viumbe hao hivyo aliamua kumpa tiba ndefu sana ambayo angesaidia kumwondoa kwenye vitabu vya kumbukumbu ya viumbe hivyo.
Aligundua hata akimtibia bado ataendelea kuandamwa na viumbe hivyo kwa sababu huyo mzee alikuwa na ushirika wa moja kwa moja na viumbe hivyo. Alikuwa akifuga majini na baadaye aliyatelekeza yakawa yanaranda randa katika mitaa ya mji wa pangani. Hapo unazungumzia majini marufu kama Chawa Mwana kawanga, jinni Barike, Makata, Kishushuna na mengine mengi ambayo ni maarufu huko Pangani.
Kwa hiyo ili aweze kupata tiba ya majini na kuachana kabisa na viumbe hao ilihitajika huduma ya mwezi mzima, huduma ambayo licha ya kuchukua mda mrefu pia ilikuwa ikihitaji pesa nyingi. Sasa ugumu ukaja mtu huyo angeshirikishwa vipi kuhusu mda wa huduma hiyo na gharama ili hali mzee huyo alikuwa hawezi kuongea.
Wazo lilokuja ni kumpigia simu mtoto wake na kumueleza hayo yanayojiri. Tariq ambaye na yeye alishapata mauaza uza ya viumbe hao kwa sasa alikuwa akiendelea vizuri na alikuwa amepata somo kuwa viumbe hivyo havitaki kufuatiliwa.
Mtaalamu alimpigia simu Tariq na kumueleza kitu kinachoendelea juu ya baba yake. Tariq kwa kuwa aliona maelezo ya kwenye simu yalikuwa ni magumu sana kuyaelewa aliamua kufunga safari na kwenda moja kwa moja mpaka visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuonana na mtaalamu huyo. Nia yake ilikuwa ni kupata ushauri wa kitaalamu kabla hawajakubali kuuza mali za mzee huyo kwa ajili ya matibabu hayo. Pesa waliotajiwa na mtaalamu huyo ilikuwa ni kubwa sana. Tariq alifunga safari na kwenda Zanbira. Akiwa huko…
***ITAENDELEA***

No comments:

Powered by Blogger.