Trending News>>

MICHEZO:Pogba kukaa nje wiki sita


Pogba alikuwa ameanza kila mechi United msimu huu

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba huenda akakaa nje ya uwanja kwa kati ya mwezi mmoja na wiki sita baada yake kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Basel Jumanne.

Mfaransa huyo wa miaka 24 alifanyiwa uchunguzi kuhusu jeraha hilo Jumatano.

Inafahamika kwamba Pogba atakosa kucheza angalau kwa mwezi mmoja.

Hilo lina maana kwamba huenda atakuwa na kibarua kujaribu kuwa sawa kucheza mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Liverpool ugenini 14 Oktoba.

Meneja wa United Jose Mourinho anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake katika kikao na wanahabari Ijumaa.

Pogba atakosa mechi za ligi dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu Jumatano dhidi ya Burton.

Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.

Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.

Ufaransa wanahitaji kushinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka ujao.

No comments:

Powered by Blogger.