Trending News>>

Siku ya nwisho ya usajili yawa kinyume na matarajio ya mashabiki..

Presha siku ya jana kwa mashabiki wengi wa Epl na ligi zingine barani Ulaya ilikuwa ni kubwa sana. Kila mtu alitarajia kununua angalau mchezaji mmoja mkubwa ili kujiweka sawa na msimu ujao.
Tetesi za dili nyingi zilitawala na zikaongeza uwezekano wa baadhi ya sajili nyingi kutokea, lakini kinyume na matarajio ya walio wengi usajili huu ulikuwa tofauti na sana na mawazo ya watu.
Manchester United wenyewe kidogo jana walikuwa kimya na hakukuwa na habari nyingi na kubwa zilizowahusu kama ilivyokuwa kwa vilabu vingine ikiwemo Manchester City, Liverpool,Chelsea,Arsenal na Barcelona.
Manchester City wenyewe tetesi zilizagaa sana kwamba wanaenda kumchukua Sanchez, baada ya kushindwa kwa muda mrefu kumnunua mshambuliaji huyo ilionekana kama City wanaweza kuikamilisha dili hiyo siku ya mwisho.
Lakini haijawa hivyo kwani Arsenal wameendelea kukaa na msimamo wao ule ule kwamba Sanchez  haendi popote na Man City wanabaki na £55m zao walizotaka kutumia kumnunulia.
Chelsea wenyewe wanaonekana kukataliwa na nyota wakubwa msimu huu akiwemo Romelu Lukaku,Chamberlain, lakini jana wakawa na matumaini kumnunua Ryad Mahrez lakini hadi sasa Mualgeria huyo ni mali ya Leicester.
Lakini Chelsea hawakutoka kapa siku ya jana kwani wamefanikiwa kumsaini Davide Zapaccosta kutoka Lazio na Danny DrinkWater kutoka Leicester City ambao wote wamewasaini usiku wa jana.
Arsenal kwa upande wao habari kubwa jana ilikuwa kuondoka kwa Sanchez na kuja kwa Thomas Lemar habari ambazozote hazijatokea, Lemar amebaki Monaco na Sanchez wamefanikiwa kubaki naye tena kwa msimu huu wa ligi.
Liverpool kwa muda mrefu walikuwa wakimuwinda Virgil Van Djik na jana ilitarajiwa angesaini Liverpool lakini wakaishia kwa Oxlade Chamberlain huku Thomas Lemar naye akishindwa kusaini katika majogoo hao wa jiji la London na pia Liverpool wakafanikiwa kuzima usajili wa Coutinho kwenda Barcelona.
Kwa ujumla dirisha limeshafungwa na kila timu imepata ilichopata japo ni ukweli uliowazi kwamba baadhi ya timu na mashabiki zao hawakuwa na furaha jinsi dirisha lilivyofungwa na walihitaji kitu kikubwa zaidi ya walichoambulia.

No comments:

Powered by Blogger.