Maiti zaokotwa Msasani beach
Wavuvi wanaovua samaki katika pwani ya Msasani Dar es salaam, wameelezea
matukio ambayo mara nyingi huwa wanakutana nayo wanapokwenda kuvua ya
kuokota maiti mara kwa mara, bila kujua ni kina nani waliowaua.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio Katibu wa Ulinzi wa Mazingira ya Pwani na Mali zake Bw. Abubakar Zumo maarufu kwa jina la Mbwembwe, amesema mara nyingi hukutana na mtukio hayo, na zile maiti ambazo wanazikuta zimeharibika huzizika moja kwa moja, huku zile zinazokuwa na afadhali, huzitolea taarifa polisi.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuokotwa kwa maiti mara kwa mara katika ufukwe wa Msasani, lakini East Africa Radio kupitia kipindi cha SUPAMIX kilipomtafuta Kamanda wa Polisi Kanda maalum Lucas Mkondya, alikiri kuokotwa kwa maiti kwa wiki mbili zilizopita.
Source: EATV

No comments:
Post a Comment