Mrembo Apata Aibu ya Mwaka!
MBEYA: Binti mmoja aliyefahamikwa kwa jina moja la Esta amejikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kuchapwa kichapo hevi na mfanyabiashara mmoja aliyedai kumuibia begi lake.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni jijini Mbeya baada Esta (pichani) kunaswa na mtu ambaye alimtuhumu kumuibia begi lake kisha kuanza kumshushia kichapo hevi kilichowakusanya watu.
Akizungumza na mwandishi wetu, mfanyabiashara huyo, alisema kuwa siku ya tukio binti huyo alifika eneo lake la kazi lililopo Stendi ya Soko Matola na kumuomba simu ili awasiliane na ndugu zake ndipo akatoweka na begi lake.
“Nilikuwa niko ofisini kwangu maeneo ya stendi akaja huyu binti akaniomba simu ili awasiliane na ndugu zake, nikampa lakini baadaye nikiwa naendelea, akanirudishia simu mimi nikiwa bize na shughuli za dukani, yeye akatoweka na begi langu lililokuwa na vitambulisho na vitu vingine.
“Nilipogundua kuwa kaniibia nikaenda kutoa taarifa kituo cha polisi ili asije akatumia vibaya vitambulisho vyangu nikaaingia matatani,” alisema mfanyabishara huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Akizidi kusimulia mkasa huo, mfanyabiashara huyo alisema baada ya kugundua kuwa binti huyo kaondoka na begi lake, aliitazama namba iliyopigwa kwenye simu na kuanza kuwasiliana na mtu ambaye alimpigia dada huyo.
“Kwa kuwa alikuwa ametumia simu yangu kuwasilina na ndugu zake nikaanza kuipiga ile namba lakini yule mtu akawa haeleweki mara anasema yuko Sumbawanga, Singida mara Mwanza, ilimradi kunichanganya tu.
“Baada ya siku kadhaa ndipo nikakutana na mwizi wangu, nikamuuliza lakini maelezo yake yakawa hayaeleweki, mara anasema begi liko Sumbawanga, Arusha mara Iringa, nilipandwa na hasira nikamchapa makofi,”alisema mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo, baada ya raia kukusanyika eneo alilokutana na mrembo huyo na kuanza kumuunganishia kichapo, alitokea msamaria mmoja na kuwasihi watu wasimpige ndipo akapandishwa kwenye bodaboda akiwa yeye na mtu aliyemuibia kuelekea kituo cha polisi.
Alisema suala hilo lilikwisha baada ya ndugu zake kusafiri kutoka Sumbawanga kisha kuzungumza naye na kumsihi asamehe ambapo walimlipa shilingi laki moja na msala ukaisha bila suala hilo kufikishwa mahakamani.
SOURCE:GLOBAL
No comments:
Post a Comment