Nashukuru wananchi mmenilipa - Roma Mkatoliki
Rapa Roma Mkatoliki amefunguka na
kudai hana deni analodaiwa na mashabiki zake mpaka sasa ila anachojua
yeye kuwa ndiyo alikuwa anawadai na ameshalipwa baada ya wao kupiga
kelele za 'free Roma' kipindi alipotoweka.
Rapa Roma Mkatoliki.
Roma
amebainisha hayo siku za hivi karibuni baada ya watu wengi kudai msanii
huyo anadeni la kulilipa kwa wananchi kwa kuwa hajazungumza jambo
lolote lililomsababisha yeye mpaka kutekwa na watu wasiyojulikana.
"Mimi ndiyo naweza kusema
niliwakopesha washkaji deni maana ndani ya miaka 10 nimeimba nyimbo za
kiharakati, changamoto pamoja kero za jamii vyote nawaimbia watu bila ya
kulipwa chochote. Leo limenikuta la kunitokea wananchi basi wameungana
kutokana na ngoma zangu wamepaza sauti zao, ukiniambia mimi nina deni ni
kama wao wamenilipa kwa sababu mimi niliwakopesha kupitia ngoma zangu",
alisema Roma.
Pamoja na hayo, Roma amesema hadhani
kama chochote atakachokieleza kwa umma wataweza kuridhika kutokana na
tukio lake jinsi lilivyokuwa.
"Sidhani kama kuna majibu
sahihi ukamwambia mtu akaridhika kuhusiana uhalisia wa tukio
lililonitokea mimi, sina cha kufanya zaidi kusema asante kwa kupaza
sauti zenu mpaka kupatikana kwangu, maisha yaendelee, nipo poa, nipo
strong, niombeeni tuendelee", alisisitiza Roma.
Video mpya ya Roma Mkatoliki 'Zimbabwe'
aliyoiachia Agosti 10 mpaka sasa imeweza kuendelea kushikilia nafasi ya
kwanza kuwa 'trending' za video katika mtandao wa Youtube.
No comments:
Post a Comment