Wanafunzi 33 watupwa Mahabusu baada ya Kulewa Pombe
WANAFUNZI
33, walimu wawili na dereva waliokuwa walevi mnamo Ijumaa walilala
ndani ya seli katika Kituo cha Polisi cha Ol Kalou, Nyandarua.
Wanafunzi hao wote walikuwa wa kidato cha nne katika shule ya mseto ya Naivasha, Kaunti ya Nakuru.
Walikamatwa Ijumaa saa tatu usiku ndani ya klabu moja kinachomilikiwa na duka la reja reja Ol Kalou.
Polisi
walipata aina tofauti za vileo na vinywaji kama soda vilivyokuwa
vimechanganywa na vileo. Walikuwa ni pamoja na wasichana 11, vijana 22
na walimu wawili wa miaka 24 na 27.
Katika kituo cha polisi, maafisa wa polisi walikuwa na wakati mgumu kuwadhibiti wanafunzi hao walioonekana walevi.
“Baadhi
ya wasichana walionekana uchi, inaonekana kuwa walikunywa siku yot.
Hawakujua kwamba wamekamatwa. Waliimba na kucheza densi za mugithi ndani
ya kituo cha polisi,” alisema afisa wa polisi.
Alisema baadhi ya wasichana walionekana kuwaalika watu wasiowajua kujiburudisha.
Msimamizi
wa polisi eneo hilo Wilson Kosgei alisema polisi walifuata gari lao
kutoka mjini Nyahururu walipodokezewa na wananchi kuwa gari hilo
lilikuwa likiendeshwa vibaya na wanafunzi walikuwa wakijihusisha na
tabia mbaya.
“Walikuwa
katika ziara ya Nakuru na baadaye Nyahururu. Waendeshaji wa magari
katika barabara ya Ol Kalou kuelekea Nyahururu walilalamika kuwa gari
lao lilikuwa likiendeshwa vibaya na wanafunzi walionekana kuwa na tabia
mbaya,” alisema msimamizi huyo.
Baada
ya kufika Ol Kalou, hawakuwa wakijua walikuwa wakifuatwa na polisi,
basi hilo lilisimama karibu na duka hilo ambapo walimu na wanafunzi
walinunua vileo zaidi.
No comments:
Post a Comment