Mwanamke mbaroni kwa Kumuua Mumewe na watoto wanne
UKIWA
bado unadhania kuwa kero za wanandoa kudhulumiana ni kero tu
lililoshamiri Kenya na pia kuwa visa vya mmoja katika ndoa kuwaua watoto
wake
kikatili ni suala la Kenya pekee, hata Marekani yanatokea.
kikatili ni suala la Kenya pekee, hata Marekani yanatokea.
Kwa
sasa, mwanamke mmoja wa Marekani ametiwa mbaroni katika taifa hilo
baada ya kudaiwa kuwa mshukiwa mkuu katika mauaji ya bwanake na watoto
wao wanne kwa kuwadunga visu.
Habari za idara ya polisi Marekani zinasema kuwa mauti hayo yalitekelezwa Alhamisi asubuhi.
Isabel
Martinez, 33, ameshtakiwa kwa makosa matano ya kutekeleza mauaji, kuua
kwa ukatili na pia kutumia mabavu katika udungaji huo wa visu katika
miili ya waathiriwa hao.
Idara hiyo inasema kuwa baada ya kutekeleza ukatili huo, mwanamke huyo alipiga simu ya dharura ya 911 kujitambulisha.
Habari hizo zinasema kuwa mwanamke huyo kwa sasa amezuliwa katika rumande ya ya Gwinnett.
Habari
hizo zinafahamisha kuwa maafisa wa kiusalama wa Gwinnett walipokea simu
ya mshukiwa huyo wa kike mwendo wa saa 4:47 ambapo ilionekana kupigwa
kutoka eneo la Emory, Loganville.
“Hakuna
shaka kuwa Martinez, na ambaye ndiye mshukiwa ndiye alipiga simu hiyo
kwetu akitufahamisha kuhusu mauaji hayo,” zasema ripoti hizo.
Wakati
maafisa hao walikimbia kuthibitisha madai hayo, wanaripoti kuwa
walipata mtoto wa tano akiwa na majeraha mabaya mwilini kando na miili
ya watano hao waliokuwa marehemu.
Maafisa hao wanaripoti kuwa wote wa watoto hao walikuwa wa chini ya umri wa miaka 10 huku baba yao akiwa wa miaka 35.
Msemaji
wa polisi wa Gwinnet, Koplo Michele Pihera ametoa taarifa akisema,
“Kile ambacho husukuma mzazi kutekeleza mauti kwa kiwango hiki kwa
watoto ambao amewazaa na kisha kuua mshirika wa uzazi wa watoto hao kwa
njia ya kikatili kiwango hiki ni suala ambalo halieleweki.”
Alisema
kuwa kitendo hicho ni “uhaini mkuu sio tu kwa waathiriwa bali pia kwa
familia yake, familia pana, jamii na taifa kwa ujumla.”
No comments:
Post a Comment