RAIS WA UMOJA WA WAKUU WA SEKONDARI ATEMBELEA SABASABA
Mkurugenzi
wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa katika
serikali ya viwanda wakuu wa shule wanaweza kujenga msingi mzuri kwa
wanafunzi kwani ni rasilimali katika sekta hiyo.
Mollel
aliyasema hayo wakati wa Rais wa Umoja wa Shule za Sekondari nchini
(Tahossa)alipotembelea banda la Global Education Link katika maonesho
ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar
es Salaam, Mollel amesema kuwa wa wakuu wa shule ndio wanaweza kuchukua
dhamana ya serikali ya kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa
serikali ya awamu katika dhana ya viwanda.
Mollel amesema kuwa serikali ya viwanda inahitaji watu wa masomo wa sayansi, sanaa na masoko kwa pamoja ndio wanajenga viwanda.
Aidha amesema kuwa Global itaendelea kushirikiana wakuu wa sekondari katika ujenzi wa nchi ya viwanda.
Naye
Rais wa Umoja wa Wakuu wa Sekondari Nchini (Tahossa) Mwalimu
Vitaris Shija amesema kuwa Global Education Link (GEL) ni chombo
ambacho kinafanya wanafunzi wapende masomo ya sayansi ambao ndio
watakaotumika katika sekta ya viwanda.
Amesema
kuwa sekta ya viwanda inahitaji wataalam wa sayansi, sanaa na biashara
ndio mahitaji ya sekta ya viwanda kwa sasa kutokana na kauli ya Rais
Dk. John Pombe Magufuli kuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali ya
viwanda.
Shija
amesema kuwa Global Education Link imeleta chachu ambapo inatakiwa
kuanza kushawishi wanafunzi kusoma sayansi kuanzia shule ya msingi
kutokana na mahitaji ya sekta ya viwanda.
Shija
amesema kuwa kutokana na mahitaji ya rasilimali katika sekta ya
viwanda wakiwa wakuu wa shule za sekondari kuzungumza suala hilo kuanzia
kwa wazazi juu ya nchi mahitaji yar rasimali katika sekta yaya viwanda.
Amesema
kuwa serikali kulipa wataalam wa nje ni gharama ambao sehemu kubwa
watalipwa na kwenda kujenga kwao lakini wanafunzi wa waliokwenda
watafanya kazi nchini na kujenga nchi yao.
Mkurugenzi
wa Global Education Link , Abdulmalik Mollel akiwa na Rais wa Umoja wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Nchini (Tahosa) Mwalimu Vitaris Shija katika
Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim
Nyerere jijini Dar es Salaam.
.Mkuu
Idara ya Masoko kwa Njia ya Mtandao, Micky Musa akionesha mfumo wa
Taarifa za wanafunzi wanaosoma nje kupitia Global Education Link (GEL)
katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha
mbalimbali za mafisa za Global Education Link (GEL) katika katika
Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim
Nyerere jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment