TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Timu
ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepanda kwa nafasi 25 hadi nafasi
114 kutoka nafasi ya 139 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa
soka duniani vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA leo Julai
6, 2017.Katika siku za hivi karibuni timu ya taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) imekuwa ikicheza katika kiwango bora kabisa
kilichoiwezesha timu hiyo kushinda katika michezo yake ikiwemo dhidi ya
Burundi na Botswana katika mchezo wa kirafiki, Malawi pamoja na Afrika
Kusini maarufu kama Bafana Bafana katika michezo ya COSAFA inayoendelea
nchini Afrika Kusini.
Katika
viwango hivyo vya mwezi Julai timu ya taifa ya Ujerumani inashika
nafasi ya kwanza, Brazili ikishika nafasi ya pili, na timu ya Argentina
ikishika nafasi ya tatu.
Mataifa mengine ambayo timu zao zipo katika kumi bora nikama zifuatazo
4.Ureno
5.Uswisi
6.Poland
7.Chile
8.Colombia
9.Ufaransa
Na nafasi ya kumi inashikiliwa na timu ya taifa ya Ubelgiji
Barani
Afrika Misri inaongoza ikiwa nafasi ya 24 ikifuatiwa na Senegal katika
nafasi ya 27, Congo DR nafasi ya 28, Tunisia nafasi ya 34, Cameroon
nafasi ya 36, Nigeria nafasi ya 39 huku Burkina Faso akiangukia nafasi
ya 44.
Kwa
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeporomoka nafasi tatu
mpaka kufikia 74, ikifuatiwa na Kenya kuanguka nafasi 10 mpaka 84,
Tanzania imepanda katika viwango hivyo kwa nafasi 25 juu mpaka kufikia
114, Burundi ikipanda nafasi 27 na kufikia 121, Rwanda imepanda nafasi
moja na kufikia 127, Ethiopia ikidondoka kwa nafasi 11 na kufikia 136.
No comments:
Post a Comment