Picha: AGPAHI YAKUTANA NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA MJINI DODOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa mkutano wa waganga wakuu wa mikoa ambako shirika hilo linafanya kazi nchini Tanzania.
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids
Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya
Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania limekutana na waganga
wakuu wa mikoa saba ambako linatekeleza shughuli zake.
AGPAHI imefanya mkutano na waganga wakuu
wa mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu,Tanga,Mara na Manyara siku ya
Jumatano, Julai 5,2017 katika ukumbi wa Morena Hotel mjini Dodoma.
Akizungumza katika mkutano
huo,Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema lengo ni
kujadiliana kuhusu maendeleo, mafanikio na changamoto za miradi na
kupanga mikakati ya utekelezaji wa miradi katika mwaka ujao wa miradi.
Dk. Mwakyusa alisema lengo la AGPAHI ni
kuboresha afya ya watoto na familia kwa kutokomeza VVU na Ukimwi na
kutoa huduma za kinga,matunzo na tiba kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa afya ikiwemo serikali ili kubuni na kutekeleza mikakati
muafaka kwa afya bora.
“Shirika hili lilianzishwa mwaka
2011,kuanzia kipindi hicho tulikuwa tunafanya kazi zetu katika mikoa ya
Shinyanga na Simiyu, lakini kuanzia Oktoba 2016 mikoa ya
Mara,Geita,Tanga na Mwanza iliongezeka (tukitekeleza miradi ya Ukimwi)
na mkoa wa Manyara uliongezeka ambako tunatekeleza mradi wa kifua
kikuu”,alisema Dk. Mwakyusa.
“Tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa
kushirikiana kwa ukaribu kabisa na serikali. Na wafadhili wetu wakuu ni
Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and
Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU kwa hisani ya Watu
wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People
(ADPP - Mozambique)”, aliongeza Dk. Mwakyusa.
Aidha alisema mbali na mapambano dhidi
ya VVU na Ukimwi pia shirika hilo linatekeleza mradi wa kifua kikuu
migodini kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu kifua kikuu kwa wachimbaji,
familia zao na jamii inayowazunguka ili waweze kuchukua hatua za
haraka kujikinga na kupata tiba sahihi ya kifua kikuu.
“Mradi huu hivi sasa unatekelezwa katika
machimbo ya Iyenze na Mwime halmashauri ya Mji wa Kahama, Kakola na
Mwazimba halmashauri ya Msalala katika mkoa wa Shinyanga pamoja na
Mererani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ”,aliongeza Dk. Mwakyusa.
Kwa upande wao waganga wakuu wa mikoa
hiyo saba walilishukuru shirika hilo kwa jitihada zake za kujali afya za
watanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana na AGPAHI ili wananchi
waweze kunufaika kupitia shirika hilo.
Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga, Dk. Asha
Mahita aliuhakikishia uongozi wa shirika hilo kuwa watakuwa wasimamizi
wazuri wa fedha zinazotolewa na AGPAHI ili kutekeleza miradi
iliyoanzishwa kwa faida ya watanzania.
“Kwanza nilipongeze shirika hili kwa
kuongeza mikoa lakini pia kuamua kutukutanisha hapa, kwa kweli huu ni
utaratibu mzuri na naomba tuendelee kushirikiana, sisi tupo tayari
kuhakikisha tunasimamia miradi iweze kutekelezeka”, aliongeza Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume.
Shirika la AGPAHI linajishughulisha na
shughuli mbalimbali kama vile kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu
wanaoishi na virusi vya Ukimwi, kutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya
virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kutoa huduma ya
uchunguzi na huduma za awali ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa
huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pia shirika hutoa vifaa
tiba, kukarabati miundombinu ya vituo vya afya, kutoa mafunzo kwa
watumishi wa afya kwa msaada wa watu wa marekani.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MKUTANO HUO
Meneja Mawasiliano kutoka AGPAHI, Jane
Shuma akiwakaribisha waganga wakuu wa mikoa katika ukumbi wa Morena
Hotel mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki mkutano ulioandaliwa na
shirika hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akielezea kuhusu miradi ya Ukimwi
inayotekelezwa na shirika hilo katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Waganga wakuu wa mikoa saba wakimsikiliza Dk. Mwakyusa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza ukumbini.Kushoto ni Mkurugenzi
wa Miradi kutoka shirika la AGPAHI, Dk. Safila Telatela.
Dk. Mwakyusa akiendelea kuelezea kuhusu miradi inayotekelezwa na shirika la AGPAHI nchini Tanzania.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk.
Rashid Mfaume( kulia) na Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk. Sungwa
Kabissi wakimsikiliza Dk. Mwakyusa.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Dk. Mwakyusa akielezea jinsi ambavyo
shirika hilo lilivyojipanga kuhakikisha kuwa watanzania wengi
wananufaika na huduma zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akiwasilisha mada kuhusu mradi wa kifua
kikuu migodini unaotekelezwa na shirika hilo katika halmashauri za
wilaya za Kahama Mji na Msalala mkoani Shinyanga na wilaya ya Simanjiro
mkoa wa Manyara.
Kaimu Mganga mkuu mkoa wa Simiyu, Dk.
Chacha Magige (kushoto) na Mganga mkuu mkoa wa Mara, Dk. Francis Mwanisi
(kulia) wakisoma taarifa mbalimbali zilizotolewa na shirika la AGPAHI
kwa kila mkoa ambako shirika hilo linafanya kazi zake.
Waganga wakuu wa mikoa wakisoma taarifa
za masuala ya VVU na Ukimwi zilizotolewa na shirika la AGPAHI. Katikati
ni Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi. Kulia ni Kaimu
Mganga mkuu mkoa wa Simiyu, Dk. Chacha Magige .Wa kwanza kushoto ni
Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Dk. Asha Mahita.
Mganga mkuu mkoa wa Mara, Dk. Francis Mwanisi akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Meneja Ruzuku kutoka AGPAHI, Umboke
Mwakilima akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya fedha za miradi
inayotekelezwa na shirika hilo.
Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga, Dk. Asha
Mahita (katikati) akichangia hoja wakati wa mkutano huo. Kulia ni Mganga
mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi, kushoto ni Mganga mkuu mkoa
wa Geita, Dk. Joseph Kisala.
Dk. Mahita akisisitiza jambo ukumbini.
Dk. Leonard Subi akichangia hoja ukumbini.
Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk. Sungwa Kabissi akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mganga mkuu mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la
AGPAHI, Dk. Safila Telatela akiwasisitiza waganga wakuu wa mikoa
kushirikiana na AGPAHI katika kufanikisha miradi ya masuala ya afya.
Dk. Telatela akisisitiza jambo ukumbini.
Picha ya pamoja: Viongozi wa shirika la AGPAHI na waganga wakuu wa mikoa ambako shirika hilo linafanya kazi zake.
Picha ya pamoja: Viongozi wa shirika la AGPAHI na waganga wakuu wa mikoa.
No comments:
Post a Comment