Serikali imepiga marufuku shule hizi
Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na mafunzo ya ufundi Mh. Profesa
Joyce Ndalichako amepiga marufuku shule ambazo hazijakamilika na kupewa
kibali kupokea wanafunzi huku akitoa mwezi mmoja kwa shule ya sekondari
Mwandiga wilayani Kigoma kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili
ipokee wanafunzi wa kidato cha tano.
Mh Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shule ya
sekondari Mwandiga ambayo inatarajiwa kupokea kwa mara ya kwanza
wanafunzi wa sayansi 143 wa kidato cha tano,ambapo ameagiza idara ya
ukaguzi kufanya ukaguzi na kutoa kibali kabla shule kupokea wanafunzi.
Mapema Mkuu wa shule ya sekondari Mwandiga Albert Mutwe alieleza kuwa
shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji,bwalo, usafiri,
nyumba za walimu na maktaba huku mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga
akiahidi kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi waweze
kuanza kidato cha tano.
No comments:
Post a Comment