Trending News>>

‘Namsikiaga Ajibu, sijawahi kumuona uwanjani’ – King Kiba

Mkali wa Bongofleva Ali Kiba ‘King Kiba’ amesema hamfahamu sana mshambuliaji mpya wa Yanga Ibrahim Ajib. King Kiba amesema kwenye mechi za Simba na Yanga watu wanaomfaham vizuri Ajib ndio walikua wakimuonesha kwamba ‘yule ndio Ajib’.
“Namsikiaga Ajibu lakini siwahi kumuona uwanjani anavyo cheza kwa sababu kwa bahati mbaya au nzuri ninapokuwa naenda uwanja wa taifa kuangalia mechi za Simba na Yanga kipindi kile wakati yupo Simba, nakua sijui hadi watu waniambie yule ndio Ajib.”
“Ni mchezaji mzuri sana nasikia yuko fresh na kipaji chake kikubwa sana, watu wanakaa wanazungumza wanampigania, wana lalamika na vitu kama hivyo kwa mchango wake mkubwa Simba.”
“Kama amekuja Yanga, namkaribisha na nitam-support.”
Ali Kiba ni shabiki mkubwa wa Yanga na amekua hafichi mapenzi yake kwa klabu hiyo na mara nyingi amehudhuria viwanjani kushuhudia mechi za Yanga.

No comments:

Powered by Blogger.