Trending News>>

Okwi kuhamia mazima Tanzania ?


Mchezaji Emmanuel Okwi.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Okwi ameamua kuja kivingine msimu huu ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake ya uwanjani ambapo sasa ameahidi kuja na familia yake yote ili iweze kumsapoti kwa karibu akiwa Tanzania na Simba.

Okwi aliyefunga ndoa kipindi cha mwaka 2012 kabla ya kuondoka Simba na baada ya hapo kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike, amesema anakuja na familia kwa kuwa kipindi hiki ana uhakika wa nyumba ya kuishi tofauti na ilivyokuwa mwanzo wakati akiitumikia klabu hiyo huku maisha yake yote alikuwa anaishi hotelini.

“Ujue maisha marefu niliyoitumikia Simba sikuwa na mke maana nilikuwa sijaoa, hivyo hata nilipoenda kucheza nje sikupata nafasi ya kwenda naye kwa kuwa tu alikuwa mjamzito lakini hata alipojifungua sikuweza kumsafirisha kwa sababu mtoto alikuwa bado mdogo" alisema Okwi
Okwi aliendelea kusisitiza kuwa atakuja na mkewe ili aweze kuona maisha ambayo huwa anaishi akiwa mbali na nyumbani

“Kutimiza furaha yangu kipindi hiki nitakuja kuishi naye ili aone kwa karibu maisha yetu tunapokuwa nje ya nyumbani maana uwepo wake naamini kabisa utakuwa ni hamasa kubwa kwangu kwani nitakuwa na muda mwingi wa kufikiria familia maana hata mtoto wangu atakuwa karibu yangu,” alisisitiza Okwi.

No comments:

Powered by Blogger.