Rais Magufuli ahaidi kuchomoa upinzani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefunguka na kuahidi kuwa bado
ataendelea kuchomoa baadhi ya watu katika vyama vya siasa nchini huku
akisema ataacha vilaza tu kwenye vyama hivyo.
Rais Magufuli
Rais
Magufuli amesema hayo leo alipokuwa kwenye ziara mkoani Tabora katika
viwanja vya Ali Hassan Mwinyi na kusema maendeleo ya nchi hayana vyama
ndiyo maana ameweza kuchangua baadhi ya viongozi kutokea upinzani na
kudai kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.
"Maendeleo hayana chama
ndiyo maana unaona nimeweza kuteuwa baadhi ya viongozi kutoka tena
kwenye chama kidogo, na nitaendelea kuchomoa watu wenye akili akili
kutoka kwenye vyama mbalimbali nitawaacha vilaza huko huko" alisema Rais Magufuli
Hata hivyo ali Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni mwanachama wa
ACT- Wazalendo ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji alifunguka
na kusema kuwa Rais Magufuli amevunja mwiko wa serikali kuwa ikiongozwa
na watu kutoka chama kimoja baada ya kumteua yeye kuwa Katibu Mkuu wa
Maji pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bibi Anna Elisha
Mghwira ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment